Saturday, December 13, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Kongamano la Kiswahili kuwavuta watafiti na wahadhiri wa kimataifa

by TNC
December 10, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Kongamano la Tisa la Kiswahili Kimataifa Kufanyika Unguja

Unguja – Kongamano la tisa la Kiswahili la kimataifa linatarajiwa kuwakutanisha wahadhiri na watafiti wa lugha kutoka mataifa mbalimbali duniani kujadili fursa za matumizi ya Kiswahili.

Kongamano hilo litafanyika siku mbili kesho na keshokutwa katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Riziki Pembe Juma amesema kongamano hilo linalenga kutoa fursa za matumizi ya lugha hiyo inayojenga jamii yenye mshikamano na upendo.

Ameeleza kuwa katika dunia ya sasa lugha hiyo haipo kwa mawasiliano pekee badala yake ni nyenzo ya kukuza elimu, uchumi, diplomasia, teknolojia na utambulisho wa mwafrika.

"Lugha ya Kiswahili inatumika kuwa ni kitega uchumi cha kuzalisha ajira kwa wadau mbalimbali," amesema Pembe.

Kongamano hilo litatoa fursa ya kujadili nafasi ya Kiswahili katika sayansi na teknolojia, umuhimu wa Kiswahili katika ujenzi wa maarifa, kuiangalia kama lugha ya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki na changamoto na fursa za ukuzaji wa Kiswahili katika karne ya 21.

Majadiliano hayo yatachangia kubuni njia mpya za kuimarisha hadhi ya Kiswahili kimataifa na kuelekeza hatua za kisera kwa lengo la kuifanya lugha hiyo kuwa chombo imara cha maendeleo ya kijamii.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (Bakiza), Dk Mwanahija Ali Juma amesema washiriki wa kongamano hilo watapata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo Zanzibar.

Tags: KimataifaKiswahilikongamanokuwavutawahadhiriWatafiti
TNC

TNC

Next Post

Quiet under pervasive fear

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company