Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Wanaotibiwa saratani nje ya nchi wapungua

by TNC
December 4, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Idadi ya Wagonjwa wa Saratani Wanaopelekwa Nje ya Nchi Yapungua

Musoma – Idadi ya wagonjwa wa saratani wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya tiba hasa bobezi imepungua kutoka wagonjwa 168 kwa mwaka katika kipindi cha miaka minne iliyopita hadi wanne kwa mwaka kwa kipindi cha mwaka jana.

Takwimu hizo zimetolewa mjini Musoma Alhamisi Desemba 4, 2025 na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa wakati akitoa taarifa juu ya ujio wa madaktari bingwa wa saratani kutoka katika taasisi hiyo, wanaotarajiwa kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kwa muda wa siku tatu.

Dk Kahesa amesema katika kipindi hicho Serikali ilikuwa ikitumia zaidi ya Sh19.4 bilioni kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa hao ambao walikuwa wakisafirishwa kwenda nchi za nje ikiwemo India, Uturuki na nyinginezo.

Uwekezaji wa Serikali Wasababisha Maboresho Makubwa

Amefafanua kuwa kupungua kwa idadi wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu kumetokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali katika sekta ya afya kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, hivyo kuwezesha sekta hiyo kutoa huduma bora zikiwamo bobezi kwa magonjwa mbalimbali ikiwamo saratani.

Ametolea mfano wa Ocean Road ambayo imepokea zaidi ya Sh60 bilioni zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kuboresha miundombinu na huduma zitolewazo hali ambayo imefanya taasisi hiyo ya kuwa kitivo cha saratani ndani na nje ya nchi nyingine za barani Afrika.

"Hata hawa wagonjwa wanne waliopelekwa nje ya nchi ni kwa sababu walikuwa wanahitaji huduma maalumu ya upandikizaji wa uboho, na habari njema ni kuwa hata huduma hiyo pia inatarajiwa kuanza kutolewa nchini hivi karibuni katika Hospitali ya Benjamin Mkapa baada ya Serikali kufanya uwekezaji mkubwa pale," amesema.

Hali ya Ugonjwa wa Saratani Nchini

Kuhusu hali ya ugonjwa wa saratani nchini, Dk Kahesa amesema hali bado sio nzuri kwani takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka wagonjwa 42,000 wapya wanagundulika kuwa na ugonjwa huo ambapo asilimia 30 ya wanatoka mikoa ya kanda ya ziwa.

Kutokana na hali hiyo taasisi yake kwa kushirikiana na Taasisi ya Global Med Care kwa ufadhili wa Serikali ya Tanzania wameamua kutoa huduma za uchunguzi wa awali sambamba na matibabu, kwenye baadhi ya hospitali zilizopo katika mikoa hiyo ya kanda ya ziwa ukiwamo wa Mara.

"Kwa hapa Mara tunapiga kambi pale Hospitali ya Wilaya ya Serengeti ambapo tutafanya uchunguzi wa ugonjwa wa saratani ikiwepo saratani ya mlango wa kizazi, matiti na tezi dume bila malipo yoyote, na kuhusu uchunguzi wa tezi dume niwaambie tu wananchi uchunguzi huu ni rafiki na unafanyika kwa njia ya damu," amesema.

Wito kwa Wananchi Kutumia Fursa ya Uchunguzi

Akizungumza kuhusu ujio wa madaktari hao, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi amewataka wakazi wa mkoa huo kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kujua hali zao za afya zao, na kwa wale ambao watabainika kuwa na viashiria vya ugonjwa wa saratani waweze kupata huduma mapema.

"Ugonjwa wa saratani ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo na habari njema ni kwamba ugonjwa huu unatibika endapo utagundulika ukiwa katika hatua za awali, hivyo niwaombe wananchi wajitokeze kwa wingi kupata huduma hii muhimu," amesema.

Amesema uboreshaji wa miundombinu katika sekta ya afya umefanyika kwa makusudi ili kuwezesha wananchi kupata huduma za afya zikiwemo bobezi katika mazingira ya karibu tofauti na ilivyokuwa awali, ambapo walilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa.

"Zamani kupata huduma bobezi ilikuwa ni changamoto watu walisafiri umbali hadi wa zaidi ya kilomita 2,000 lakini sasa hivi Serikali imeleta vifaa hadi ngazi ya hospitali za wilaya, hivyo kuwezesha madaktari bingwa na bobezi kufika katika maeneo hayo na kutoa huduma kwa wananchi," amesema Kanali Mtambi.

Kanali Mtambi amesema wagonjwa watakaobainika kuwa na viashiria vya awali watapatiwa matibabu na kwa wale ambao watakuwa wamefikia hatua za juu watapewa rufaa kwenda kupata matibabu zaidi katika hospitali za ngazi ya juu, hivyo ni vema wananchi wakatumia fursa hiyo kwa ajili ya kujua afya zao.

Tags: NchinjesarataniWanaotibiwawapungua
TNC

TNC

Next Post

Authorities arrest lovers in first seizure of drugs linked to serious crimes

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company