Monday, December 8, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Kesi ya kughushi vibali vya silaha inayowakabili maafisa wa polisi, yaendelea

by TNC
November 24, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Upelelezi wa Kesi ya Kughushi Vibali vya Silaha Umekamilika

Dar es Salaam – Upelelezi wa kesi ya kughushi vibali vya kumiliki silaha inayowakabili watu tisa wakiwemo maofisa sita wa Jeshi la Polisi, umekamilika.

Wakili wa Serikali, Roida Mwakamele leo Jumatatu Novemba 24, 2025 ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili kutajwa.

Wakili Mwakamele ametoa taarifa hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geofrey Mhini, anayesikiliza kesi hiyo.

Washtakiwa

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mkaguzi wa Polisi mwenye namba PF. 19931 Fredrick Malekela (45) mkazi wa Kilwa Road, E. 4627 Sajenti Kalemwa Kaunga (54) mkazi wa Chanika, E.7855 Sajenti Edger Mlogo (54) mkazi wa Kibamba, F.1126 Sajenti Robert Titus (47) mkazi wa Kisarawe, F.5092 Sajenti John Kaposwe (46) mkazi wa Kurasini na WP 10050 Julieth Moshi (30) mkazi wa Kisarawe.

Wengine ambao sio maofisa wa jeshi hilo ni Damson Mnyilenga (59) mkulima na mkazi wa Chanika, Simon Aloyce (60) mfanyabiashara na mkazi wa Mwanza pamoja na Venrand Liberio (29) mfanyabiashara na mkazi wa Tataba.

"Mheshimiwa hakimu, kesi imeitwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi umekamilika, hivyo tunaomba mahakama itupangie tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea hoja za awali (PH)," amesema Mwakamele.

Tatizo la Mshtakiwa Mmoja

Wakili Mwakamele baada ya kutoa taarifa hiyo, wakili wa utetezi George Mwalale amedai mshtakiwa F.5092 Sajenti John Kaposwe (46) yupo Dodoma ana kesi nyingine ya utakatishaji fedha na leo hajafika Mahakamani hapo.

Hivyo aliomba siku ya kusomwa hoja za awali, mteja wake huyo Kaposwe apelekwe Mahakama hapo.

Hata hivyo, hakimu Mhini amemueleza wakili kuwa lazima Mahakama ya Kisutu ipate namba ya kesi ya mshtakiwa huyo huko aliposhtakiwa ili wajiridhishe baada ya hapo, hatua nyingine zitafuata.

Hakimu Mhini baada ya kueleza hayo, alikubaliana na upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 16, 2025 watakaposomewa hoja za awali.

Washtakiwa wapo nje kwa dhamana isipokuwa mshtakiwa Kaposwe, ambaye ana kesi nyingine mkoani Dodoma.

Maelezo ya Mashtaka

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 18451 ya mwaka 2025, yenye mashtaka 16 ya kughushi vibali vya kumiliki silaha.

Washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kutenda makosa hayo, kinyume na kifungu namba 333 na 335A na kifungu 337 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Katika mashtaka yao, wanadaiwa kuwa vibali hivyo, vimetolea kati ya Desemba 5, 2024 hadi Aprili 4, 2025.

Katika shtaka la kwanza, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa katika kipindi cha mwaka 2024, ndani ya Jiji la Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya walitengeneza nyaraka ya uongo ambayo ni kibali cha kumiliki silaha cha Desemba 5, 2024 chenye jina la Ahmed Ally, wakati wakijua kuwa sio kweli.

Shtaka la pili hadi la 13, washtakiwa wanadaiwa katika kipindi cha mwaka 2024 ndani ya mkoa wa Dar es Salaam, walitengeneza vibali vya kumiliki silaha vyenye majina ya Ahmed Ahmed Sandrudin, Omary Abdallah, Robert Koka, Fathi Ally, Mohamed Salim, Suleman Mbewa, Mickdad Chakindo, Irfan Nafari, Gulam Abbas Najafi, Ismail Ismail na Salim Salim.

Shtaka la 14 hadi 16, washtakiwa hao wanadaiwa mwaka 2025 katika mkoa wa Dar es Salaam, kwa nia ya kulaghai walitengeneza nyaraka za uongo ambazo ni kibali cha kumiliki silaha chenye jina la Marwaan Habretsh, Maurice Kitiwe na Said Mohamed, wakati wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Julai 28, 2025 na kusomewa mashtaka hayo ambayo waliyakana na wapo nje kwa dhamana.

Tags: inayowakabilikesikughushimaafisaPolisisilahaVibalivyayaendelea
TNC

TNC

Next Post

Renovation of historic MV Liemba reaches 42 percent

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company