Monday, December 8, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Suala la SUK bado, vigogo wajifungia kujadili

by TNC
November 23, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

ACT-Wazalendo Yafanya Kikao cha Dharura Zanzibar Kujadili SUK

Dar es Salaam – Kamati ya Uongozi ya Chama cha ACT-Wazalendo imejifungia kwa siku moja visiwani Zanzibar kujadili masuala mbalimbali ikiwamo tathmini ya hali ya kisiasa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

TNC imepata taarifa kuwa kikao kinaweza kujadili na kutoa uamuzi wa chama hicho kuingia au kutoingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ambayo ipo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 iliyofanyiwa maboresho mwaka 2010.

Kikao cha kamati ya uongozi ni cha kwanza kufanyika tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu na kuongozwa na Dorothy Semu (kiongozi wa chama) pamoja na wajumbe waandamizi akiwamo Zitto Kabwe, Othman Masoud (mwenyekiti wa chama) na Ado Shaibu (katibu mkuu).

Katika kikao kilichofanyika katika ofisi ndogo za makao makuu ya ACT-Wazalendo, Vuga Mjini Unguja, chama hicho kimetoa picha zinazowaonesha viongozi wao wakiendelea na kikao hicho bila kueleza kwa kina ajenda za kikao hicho.

Kwa kawaida kamati ya uongozi huwa na vikao vinavyotoa uamuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mwenendo wa chama hicho.

Mashauri 25 Mahakamani

Kufanyika kwa kikao hicho kumetanguliwa na mfululizo wa matukio mbalimbali yakiwamo mwanasheria mkuu wa chama hicho, Omar Said Shabaan kutangaza kuwa ACT-Wazalendo itafungua mashauri 25 katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kupinga matokeo ya uchaguzi ya uwakilishi na ubunge.

Kesi hizo zinahusisha majimbo ya uchaguzi 25 kati ya 50 yaliyopo Pemba na Unguja.

Katika uchaguzi huo, ACT-Wazalendo ilishinda majimbo 10 huku Chama cha Mapinduzi (CCM) ikishinda majimbo 40 kati ya 50 yaliyopo Zanzibar.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman amekuwa na mfululizo wa ziara za kuzungumza na wanachama na viongozi wa chama hicho Pemba na Unguja kujadili yaliyojiri siku ya uchaguzi mkuu.

Kwa nyakati tofauti Othman amekuwa akieleza wazi kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi huo, hata hivyo amewataka wanachama kuwa watulivu katika kipindi hiki, akisisitiza chama hakitafanya uamuzi wa kujiunga na SUK bila kuwashirikisha.

Othman alisema ACT-Wazalendo itaendelea kusimama kudai uchaguzi huru, haki na ushirikishwaji wa kweli wa wananchi katika uamuzi unaohusu mustakabali wa Taifa.

Matokeo ya Uchaguzi

Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025 ulioshindaniwa na wagombea 11 wa kiti cha urais, Dk Hussein Mwinyi wa CCM alishinda kwa kura 448,892 sawa asilimia 74.8 akifuatiwa na Othman aliyepata kura 139,399 sawa na asilimia 23.22.

Novemba 13, 2025 akihitimisha ziara yake Pemba, Othman alifichua namna ACT-Wazalendo walivyoandikiwa barua na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Zena Said inayowataka kupeleka jina la Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Akizungumzia hilo, Othman alisema hawajapeleka jina hilo hadi sasa kwa madai ya kutoridhika na mazingira ya kisiasa yaliyopo visiwani humo.

Hata hivyo, siku hiyo hiyo, Rais Mwinyi alitangaza baraza lake la mawaziri huku akiacha nafasi za wizara nne zikiwa ni maalumu kwa ajili ya ACT-Wazalendo ambacho ndio chama cha upinzani visiwani humo.

Wizara Nne Zimewekwa Wakfu

Wizara hizo ni Utalii na Mambo ya Kale, Afya, Biashara na Maendeleo ya Viwanda na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar.

Dk Mwinyi alisema nafasi hizo zitakuwa wazi kwa siku 90 kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na kama ACT-Wazalendo hawatapeleka majina, atateua kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya siasa wamesema uwepo wa kikao cha kamati ya uongozi chenye wajumbe zaidi ya 10 unaongeza joto la kupata ufumbuzi wa ACT-Wazalendo kuingia au kutoingia SUK.

Inaelezwa kuwa kauli za Dk Mwinyi za hivi karibuni zinaongeza chachu kwa viongozi wa chama hicho kufanya uamuzi chanya kuhusu SUK, ikizingatiwa Othman ameshafanya ziara ya kusikiliza wanachama kuhusu yaliyojiri.

Novemba 10, 2025 akizindua Baraza la Wawakilishi, Dk Mwinyi alisema yupo tayari kutekeleza maridhiano na kuunda SUK.

"Nitaheshimu maridhiano na nipo tayari kuyatekeleza na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984," alisema Dk Mwinyi.

Tags: BadoKujadiliSualaSUKVigogowajifungia
TNC

TNC

Next Post

Serikali yajibu wasiopata miili ya ndugu, jamaa zao

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company