Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Wajasiriamali wafichua siri ya tiba kwenye maua

by TNC
November 22, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Maua: Manufaa ya Kiafya Ambayo Wengi Hawajafahamu

Morogoro – Wajasiriamali wa bidhaa za maua katika Maonesho ya Biashara ya Morogoro wamesema kuwa, licha ya maua kutambulika zaidi kama mapambo ya nyumba, bustani na hoteli, yana pia manufaa makubwa kiafya ambayo sehemu kubwa ya jamii bado haijayafahamu vya kutosha.

Mjasiriamali wa maua na mimea tiba, Neema Katendele, amesema maua yana thamani inayozidi uzuri wake wa nje, kwani baadhi ya aina hutumika kama tiba asilia kwa magonjwa mbalimbali ya binadamu.

Neema amebainisha kuwa maua yanapohifadhiwa na kutunzwa vizuri yana uwezo wa kuboresha ubora wa hewa ndani ya nyumba, kutuliza mazingira, kupunguza mfadhaiko na kuongeza ustawi wa kimwili na kiakili.

Ameongeza kuwa baadhi ya maua husaidia kupunguza au kutibu matatizo kama vidonda vya tumbo, presha ya kupanda na kushuka, matatizo ya masikio, pamoja na kuondoa msongo wa mawazo.

"Maua yana faida nyingi kwa afya ya binadamu. Hasa maua ya msharifu, ‘rosemary’ na mchaichai. Msharifu hutibu vidonda vya tumbo na kisukari, ‘rosemary’ hutibu presha, na mchaichai hutibu uchovu wa mwili," amesema Neema.

Mjasiriamali mwingine wa maua, Idda Maro, ameeleza kuwa tabia za maua zinatofautiana kulingana na mazingira yao ya ukuaji.

Baadhi hupenda jua muda wote, wengine kivuli au mchanganyiko wa yote mawili, ili kuleta mafanikio ya kipekee.

"Maua huleta nuru, furaha, upendo, na utulivu katika nyumba. Watu wanaoishi katika maeneo yenye maua huiga tabia ya kuvutia na kupata mazingira bora," amesema Idda.

Meneja wa Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA) Mkoa wa Morogoro, Dustan Mziwanda, amesema kuwa maonesho hayo ni fursa ya kipekee kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wa mkoa huo kuonyesha ubunifu na bidhaa zao.

"Tumeshanza kugawa mabanda kwa wajasiriamali waliothibitisha kushiriki. Wajasiriamali wataanza shughuli zao za kutangaza biashara na kutoa elimu kwa wananchi," amesema Mziwanda.

Tags: KwenyemauaSiritibaWafichuaWajasiriamali
TNC

TNC

Next Post

Balozi atoa maagizo matano sekta ya bandari

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company