Monday, December 8, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mvua ya masaa sita yasababisha usumbufu jijini Mwanza

by TNC
November 21, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mvua Kali Yasababisha Mafuriko na Usumbufu wa Usafiri Mwanza

Mwanza. Mvua iliyonyesha kwa zaidi ya saa sita tangu saa 1 asubuhi leo Ijumaa Novemba 21, 2025 imewasababishia adha watumiaji wa njia inayokatisha daraja la Wakoma jijini Mwanza baada ya daraja hilo kufurika maji.

Huo ni mwendelezo wa maji kupita juu ya daraja hilo pindi Mto Mirongo unapojaa maji.

Baadhi ya barabara zilizoathirika ni ile ya U-turn na Uhuru ambazo zinapita juu ya Mto Mirongo.

Kutokana na mvua hiyo na madaraja kuzidiwa na kusababisha maji kupita juu yake, kumesababisha usumbufu kwa watumiaji wa maeneo hayo zikiwemo daladala, bajaji na watembea kwa miguu, ambapo baadhi ya vyombo hivyo vya usafiri vimelazimika kubadilisha njia za safari zao.

TNC imeshuhudia watembea kwa miguu wakipata taabu kupita katika eneo la daraja la Wakoma katika barabara ya Uhuru ambayo imejaa maji na tope kutokana na mvua hiyo.

Mmoja wa wananchi katika eneo hilo, Joseph Marwa amesema hali hiyo imekuwa ya kudumu kwa miaka mingi lakini mamlaka za Serikali zimekuwa hazichukui hatua zozote.

"Hili siyo jambo geni hapa kila mwaka mvua ikinyesha hali ni hii na mamlaka zinafahamu na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa, huwa wanasubiria tope likauke ndipo waje walitoe, hivyo tumezoea," amesema Marwa.

Naye, Magdalena Sylvester ameiomba Serikali kuitazama kwa jicho pana changamoto hiyo kwa kuhakikisha wanaliinua daraja la Wakoma ili maji yasipite juu na kuleta usumbufu.

Hata hivyo, mwaka 2022, Serikali iliahidi kujenga kingo za Mto Mirongo kwa kutenga zaidi ya Sh9.2 bilioni kujenga na kuimarisha kingo za mto huo unaokatisha katikati ya Jiji la Mwanza kuondoa adha ya mafuriko yanayotokea nyakati za masika na kuwaacha wakazi wa jiji hilo na kilio cha uharibifu na upotevu wa mali.

Mto Mirongo unaokusanya maji kutoka Wilaya za Magu, Kwimba na baadhi ya maeneo ya Wilaya za Nyamagana na Ilemela, humwaga maji yake ndani ya Ziwa Victoria na imekuwa ikifurika mara kwa mara kipindi cha masika huku maji yake yakisambaa na kusomba mali na bidhaa za wafanyabiashara katika mitaa ya Mabatini, Nera, Liberty na Uhuru jijini Mwanza.

Katika mafuriko hayo, maji ya mto huo pia hufurika hadi kupita juu ya daraja la Wamaasai katika barabara ya Uhuru na kukatisha mawasiliano kati ya barabara ya Uhuru, Liberty na Kenyatta.

Pamoja na kusomba bidhaa zinazowekwa nje ya maduka ya jumla na rejareja katika mitaa ya Nera na Liberty jijini Mwanza, mafuriko ya Mto Mirongo pia husababisha mitaa kadhaa na barabara ya Uhuru kufungwa kutokana na maji kupita juu ya daraja la Wamaasai.

Tags: jijinimasaaMvuaMwanzaSitausumbufuyasababisha
TNC

TNC

Next Post

Police warn against incitement as Tanzania tightens security surveillance

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company