Monday, December 8, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Wananchi wapiga mawe gari ya Zimamoto, DC aingilia kati

by TNC
November 20, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Moto Uteketeza Nyumba ya Makazi na Biashara Shinyanga

Shinyanga – Novemba 19, 2025 saa 12 jioni nyumba yenye makazi ya watu na biashara iliyopo maeneo ya Mnara wa Voda, mkoani Shinyanga iliteketea kwa moto.

Wananchi walifanikiwa kuuzima moto huo wakidai gari la zimamoto lilichelewa kufika eneo la tukio na kuchukua hatua ya kulishambulia kwa mawe.

Wakizungumza Novemba 19, 2025 baadhi ya mashuhuda na waathirika wa ajali hiyo wameeleza kusikitishwa na kitendo cha polisi kuondoa watu kwa silaha wakidai hao ndio waliotoa msaada mkubwa katika kuokoa mali zilizokuwa ndani ya nyumba iliyokuwa inawaka moto.

"Watu hawa wamekuja baada ya mimi kupiga kelele kuomba msaada, wametoa msaada mkubwa katika kuokoa vitu pamoja na kuzima moto, nimepigia zimamoto muda mrefu sana hawaonekani na ofisi yao ilipo sio mbali na hapa, ni hapo tu nyuma ya shule, kwa hiyo ni kosa wao kuja kuokoa hadi polisi waanze kuwapiga mabomu," amesema Zainab Shaban.

"Moto ulianza saa 11 jioni, zimamoto tumewafuata ofisini kwao wanasema tunakuja! tunakuja! Tukaanza kuokoa chumba hadi chumba na baadhi ya vyumba vimeteketea, lakini tumeshangaa askari wanafika wanaanza kupiga watu mabomu wakati vitu hivi vyote vimeokolewa na watu, hapa kuna watoto, wenye presha na wazee vipi kama wangeumiza watu," amehoji Said Ramadhan.

Mmoja wa ndugu wa familia iliyopata ajali, Baby Mohammed ameeleza kuwa alipigiwa simu akiwa kwake wakati anakuja alipita ofisi ya zimamoto kuomba msaada lakini gari la zimamoto likawa haliwaki.

"Nyumba iliyoteketea moto ni ya baba mdogo, nilipigiwa simu nikiwa nyumba Ndala, nikiwa njiani nakuja nikapita zimamoto kuomba msaada wa gari, wakasema linagoma kuwaka baadaye likawaka ndio wakaja, wakati nafika hapo nimekuta moto umepungua, nawashukuru wananchi kwa juhudi zao za uokoaji japo mzigo mkubwa umeteketea, hii nyumba ina vyumba vitano vya kuishi upande wa nyuma na mbele vyumba vitano vya biashara," amedai Baby.

Mkuu wa Wilaya Atoa Onyo

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro amewaonya vijana kutorudia tena kushambulia gari la zimamoto kwa sababu likiharibika hakutakuwa na msaada wa vyombo vya kuzimia moto, na bado litanunuliwa kwa kodi za wananchi itakuwa ni hasara.

"Familia iliyoathirika itapatiwa msaada na kilichotokea leo kisijirudie kuna watu wachache ambao wameanzisha na wengine wakafuata mkumbo, hapa katika wilaya yetu kuna gari moja tu la zimamoto tusichukue hatua mkononi bila ya kujua ni changamoto zipi zimetokea, na hapa katika eneo hilihili ni mara ya pili baada ya miezi michache tukio kama hili linatokea, nimetoa maagizo kwa kamati husika kufanya uchunguzi," amesema Mtatiro.

Pia amesema, "Nawaambia kwa sababu ni kama vijana wenzangu kuna watu wamepanga kufanya maandamano Desemba 9, nawaombeni kuweni watulivu kama mlivyofanya kipindi kilichopita msifuate mkumbo, mkifuata mkumbo tutakaa nyumbani hakuna shughuli zitakazo endelea na wafanyabiashara tutapata hasara."

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amesema askari watakuwa eneo la tukio kwa kulinda wananchi na mali zao hasa kwa mali ambazo zimeokolwa.

"Tuko hapa eneo la tukio kuweka ulinzi kwa ajili ya usalama wa raia na mali zilizookolewa, lakini Jeshi la Zimamoto litafanya uchunguzi kujua chanzo cha ajali hiyo ya moto ni nini, pia tunapita kwa familia kujua na kufanya tathmini ya vitu gani vilivyoharibika na kwa kiasi gani," amesema Magomi.

Tags: aingiliaGariKatimaweWananchiWapigaZimamoto
TNC

TNC

Next Post

Leader renews call for local leadership in major projects

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company