Dar es Salaam – Baadhi ya tovuti duniani pamoja na aplikesheni kama X, PayPal na ChatGPT leo Jumanne zimepitia changamoto ya kushindwa kufanya kazi kutokana na hitilafu iliyojitokeza kwenye miundombinu ya intaneti ya kampuni ya Cloudflare.
Cloudflare ni kampuni inayosaidia tovuti kulinda na kudhibiti trafiki ya intaneti. Kazi kuu ya Cloudflare ni kusaidia kulinda na kuharakisha rasilimali za intaneti.
Ilianzishwa mwaka 2009 kwa lengo la kudhibiti barua taka (email spams) lakini imebadilika na leo inahudumia mamilioni ya watumiaji kwa kutumia DNS na huduma za usalama.
Cloudflare leo imesema tatizo lilianzia saa 6:30 asubuhi likisababishwa na faili la mipangilio (setting file), lililotengenezwa ki-otomatiki kwa ajili ya kudhibiti vitisho vya kiusalama.
TNC imeelezwa kuwa faili hilo lilikuwa kubwa kupita kiasi na kusababisha mfumo wa kushughulikia mtiririko wa data kuanguka, jambo lililosababisha huduma kadhaa kushindwa kufanya kazi.
Katika changamoto hiyo baadhi ya watumiaji wameshindwa kufungua tovuti kwani wamekutana na ujumbe wa Cloudflare error.
Ujumbe uliokuwa unajitokeza ukifungua aplikesheni au tovuti mbalimbali ulikuwa unasema "Please unblock challenges.cloudflare.com to proceed". Wengine walipokea jumbe za Error wakati wanapanga mitandaoni.
Kwa sasa mtandao huo umerudi kawaida na watu wanaweza kutumia aplikesheni au tovuti mbalimbali kama kawaida kwani changamoto hiyo iliyojitokeza kuanzia muda wa asubuhi mpaka jioni imetatuliwa.
Cloudflare wamefahamu na wamechunguza suala hilo kwa undani ambalo hakuathiri wateja wengi.
Hata hivyo kampuni hiyo imehakikisha baadhi ya mifumo itaendelea kupata changamoto huku ikijitahidi kutatua matatizo ya kiufundi yanayowakabili.
Changamoto hii inakuja ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kukatika kwa huduma za wavuti za Amazon ambapo tovuti na programu zaidi ya 1,000 zilikatika nje ya mtandao.
Mtoa huduma mkuu wa huduma za wavuti, Microsoft Azure, pia aliathiriwa muda mfupi baadaye na tatizo hilo.