Monday, December 8, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Polisi wakiri kumshikilia daktari aliyedaiwa kutekwa, waziri wa afya atoa kauli

by TNC
November 19, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Polisi Geita Wamkamata Dk Kibaba Michael Kwa Tuhuma za Kijinai

Geita – Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limekiri kumkamata Dk Kibaba Michael kutokana na tuhuma mbalimbali za kijinai ambazo hazijawekwa wazi, ambapo imeelezwa kuwa tayari uchunguzi umekamilika dhidi yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano Novemba 19, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo, jeshi hilo limekiri kumshikilia daktari huyo kwa makosa ya kijinai yanayomkabili.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limemkamata na linaendelea kumuhoji Dk Kibaba Michael, mkazi wa Manispaa ya Geita. Sababu za kumkamata ni kutokana na ushahidi uliokuwa umekusanywa kuhusiana na tuhuma mbalimbali za kijinai anazotuhumiwa nazo.

Taarifa hiyo bila kuwataja watu wengine anaoshirikiana nao katika makosa hayo ya jinai, imeeleza kuwa linakamilisha uchunguzi ili mtuhumiwa huyo achukuliwe hatua za kisheria pamoja na anaoshirikiana nao.

"Uchunguzi uliobakia unakamilishwa ili hatua nyingine za sheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake na anaoshirikiana nao," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kauli ya jeshi hilo inakuja baada ya kuibuka kwa taarifa katika mitandao ya kijamii ikieleza kuwa Dk Kibaba Furaha anayefanya kazi katika Hospitali ya Manispaa ya Geita akiwa mratibu wa mpango wa kudhibiti Malaria, kudaiwa kutekwa na watu wasiojulikana. Pia ilidaiwa kuwa Dk Kibaba alivamiwa na watu waliokuwa na silaha akiwa katika kibanda chake cha biashara mtaa wa Aziboni na kuondoka naye, huku watu hao wakichukua pia simu yake na kompyuta mpakato aliyokuwa nayo.

Rais wa Chama cha Madaktari nchini, Dk Mugisha Nkoronko amekiri kupokea taarifa hiyo, ambapo amesema kuwa wamekuwa wakifanya ufuatiliaji kupitia Jeshi la Polisi na kulitaka jeshi hilo kumfikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria.

"Kwa kuwa ni mambo ya kijinai, tunataka Polisi iendelee na shughuli zake kwa uwazi ikiwemo kumfikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria, ndiyo tutajua makosa yake yanaangukia kwenye eneo gani."

"Kwa kuwa taarifa ya Jeshi la Polisi imeeleza inamshikilia, tofauti na hapo nyuma ilivyokuwa, tunashukuru kusikia kuwa ni mzima na tuendelee kuwataka wenzetu wanaotekeleza sheria kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Polisi, kukamilisha utaratibu wa kumshtaki rasmi ufuatie, tunaendelea kushirikiana na familia pamoja na wadau wenye nia njema na taaluma ya udaktari kuona haki inatendeka kwa daktari mwenzetu," amesema Dk Nkoronko.

Tags: AfyaaliyedaiwaatoadaktariKauliKumshikiliakutekwaPolisiwakiriWaziri
TNC

TNC

Next Post

President lands in Dar for mediation amidst debate

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company