Saturday, March 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Sajenti wa Jeshi akamtwa akiwa na mabomu manne

by TNC
November 17, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Sajenti wa Jeshi la Marekani Akamatwa na Mabomu Mpakani Mwa Tanzania-Kenya

Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Tarime–Rorya mkoani Mara limemkamata Sajenti wa Jeshi la Marekani, Charles Onkuri Ongeta (30), mwenye uraia pacha wa Marekani na Kenya, baada ya kukutwa na mabomu manne ya kurushwa kwa mkono aina ya CS M68 katika eneo la mpakani Sirari.

Tukio hilo limetokea Jumapili, Novemba 16, 2025, saa 6:00 mchana, wakati askari wa ulinzi mpakani walipomuhoji mtuhumiwa aliyekuwa akiingia Tanzania akitokea Kenya na gari aina ya Toyota Land Cruiser.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime–Rorya, Mark Njera, imeeleza kuwa kukamatwa kwa mtuhumiwa kumetokana na umakini wa askari waliokuwa doria mpakani.

"Askari wetu walifanya ukaguzi wa kawaida na ndipo walipobaini uwepo wa mabomu manne ya kurushwa kwa mkono ndani ya gari alilokuwa akiendesha mtuhumiwa," amesema Kamanda Njera.

Ameongeza kuwa silaha hizo ni marufuku kuingizwa nchini kwa mujibu wa sheria za Tanzania hata kama angekuwa ameomba kibali maalumu.

"Kwa mujibu wa sheria ya umiliki wa silaha, mabomu ya aina hii hayaruhusiwi kabisa kuingizwa nchini. Hata kama angeomba kibali, asingeruhusiwa kuyapitisha," amefafanua.

Kamanda Njera amesema uchunguzi wa awali unaendelea, ikiwa ni pamoja na kukusanya ushahidi na kumuhoji mtuhumiwa, ili hatua za kisheria zichukuliwe baada ya taratibu kukamilika.

"Tunachukua hatua zote za kipolisi. Mara tu uchunguzi utakapokamilika, tutawasilisha jalada kwa mamlaka husika kwa ajili ya hatua zaidi," amesema.

Tags: akamtwaAkiwaJeshimabomumanneSajenti
TNC

TNC

Next Post

Tumepiga hatua kidemokrasia, lakini umaskini bado

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company