Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Samia: Tanzania iheshimiwe kama inavyoheshimu wengine

by TNC
November 15, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dar es Salaam – Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania kama Taifa linapenda liheshimiwe kama linavyoheshimu mataifa mengine na katika kulinda masilahi ya nchi, hakuna mbadala.

Amesema lazima kuhakikisha tunalinda utu, uhuru, na heshima ya Taifa letu na kwamba nchi itaendelea kuongozwa kwa misingi ya sera ya nje iliyoasisiwa na waasisi ya kutofungamana na upande wowote.

Rais Samia ametoa msimamo huo leo, Ijumaa Novemba 14, 2025 alipozungumza katika hotuba yake ya kulifungua Bunge la 13, jijini Dodoma.

"Msimamo wetu ni umoja na ushirikiano badala ya mgawanyiko, majadiliano badala ya amri au mabavu na haki badala ya visasi," amesema.

Amesema Tanzania imejengwa katika misingi ya amani na utulivu wa kisiasa na haitakubali nguvu yoyote inayokusudia kuchafua misingi hiyo.

Ametumia jukwaa hilo kuweka wazi kuwa Serikali yake itaendelea kuviimarisha vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha mipaka na raia wanalindwa vema.

Amesema Tanzania itaendelea kutimiza wajibu wake wa kuchangia misheni za ulinzi wa amani za kikanda na kimataifa.

"Msingi wa mafanikio ya yote haya ni utawala wa sheria, uadilifu na uwajibikaji kuanzia juu hadi chini. Kufanikiwa kwa yote tuliyoyasema ni kuwa na misingi imara kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali za nchi pamoja na kupata huduma wanazostahili," amesema.

Amesema Serikali yake itaelekeza jitihada zake kwenye mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi, ubadhilifu, uzembe, ukosefu wa nidhamu na maadili.

Amesema lazima wachache wanaotaka kuirudisha nchi kwa kuendekeza masilahi binafsi wadhibitiwe.

Ili kuimarisha uwajibikaji serikalini, amesema ataendeleza kutekeleza programu za maboresho ya utumishi wa umma ikiwemo matumizi ya mifumo ya upimaji wa utendaji kazi.

"Wajibu huendana na haki na haki huendana na wajibu. Hivyo, pamoja na kuwataka watumishi wawajibike, tutaendelea kuboresha masilahi yao kwa kadri uchumi utakavyoruhusu," amesema.

Ameeleza Serikali yake itaimarisha uwajibikaji na utendaji wa mashirika ya umma, ili kuboresha ufanisi, uwazi na tija na anachotaka kuongeza sio tu gawio bali kuchangia angalau asilimia 10 ya mapato yote.

Tags: iheshimiweinavyoheshimukamaSamiaTanzaniaWengine
TNC

TNC

Next Post

Tanzania's path to democracy will be guided by consensus, not external pressure, says Samia

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company