Monday, December 8, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Bei za mafuta zapaa Zanzibar

by TNC
November 9, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Bei za Mafuta Zaongezeka Zanzibar, Mafuta ya Taa Yasalia

Unguja – Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (Zura) imetangaza kupanda kwa bei za mafuta isipokuwa mafuta ya taa pekee.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 8, 2025, bei mpya zinaanza kutumika Novemba 9, 2025.

Mkurugenzi Mkuu wa Zura, Omar Ali Yussuf, amesema lita moja ya petroli kwa Novemba itauzwa Sh2,868 kutoka Sh2,809 ya Oktoba sawa na ongezeko la Sh59.

Pia, bei ya dizeli itakuwa Sh3,004 kutoka Sh2,944 sawa na ongezeko la Sh60 huku mafuta ya taa pekee yakisalia kwenye bei yake ya Sh3,000.

Taarifa hiyo imeeleza kupanda kwa mafuta ya ndege kutoka Sh2,343 ya Oktoba hadi kufikia Sh2,405 sawa na ongezeko la Sh62.

"Sababu za kupanda kwa bei za mafuta kwa Novemba inatokana na kupanda kwa gharama za uingizaji wa bidhaa za mafuta kutoka soko la Dunia hadi kufika Zanzibar," imesema taarifa hiyo.

Shirika la Bandari Lapunguza Tozo

Bei hizo zinapanda wakati ambapo Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) limepunguza asilimia 80 ya tozo ya aridhio (wharfage) kwa bidhaa zote za chakula zinazoingia nchini kupitia bandari zote zinazohudumiwa na Shirika hilo.

Punguzo la ushuru hicho ni kuweka uhimilivu wa bei za bidhaa hizo ambazo zinatajwa kuvurugika kutokana na machafuko yaliyotokea siku ya upigaji kura Oktoba 29, 2025.

Kwa takribani siku tano, usafiri na usafirishaji vilisitishwa kuingia na kutoka Zanzibar, ikikumbukwa kuwa bidhaa nyingi za vyakula zinazotumika Zanzibar zinaingizwa kutoka Tanzania bara.

Mkurugenzi Mkuu wa ZPC, Akif Ali Khamis alisema punguzo hilo linahusu bidhaa za vyakula vinavyotoka Tanzania na sio nje ya nchi.

Alisema hilo ni kutokana na kwamba tayari walitoa asilimia 100 ya Uhifadhi wa bidhaa kutoka nje ya nchi kwa siku zile ambazo bidhaa zilishindwa kuingizwa.

Wananchi Wahofia Ongezeko la Gharama za Maisha

Wakizungumza kuhusu kadhia hiyo baadhi ya wananchi wamesema huenda gharama za maisha zikapanda zaidi baada ya mafuta kuongezeka bei kwani mambo mengi yanategemea mafuta.

"Hizi ni dalili mbaya kwa kweli, maana mafuta yakishapanda kila kitu kinapanda, na ukiangalia katika mazingira tuliyonayo kwa sasa hata bei za bidhaa nyingine sio rafiki," amesema Juma Mtumwa Juma mkazi wa Magogoni Zanzibar.

Mwananchi mwingine, Alkadir Mahmoud amesema: "Ndio maana watu wanaishauri kuwa na stock kubwa ya mafuta nchini kuliko kutegemea kuagiza mafuta ya kila mwezi na hizi ndio athari na wanaoumia ni wananchi wa hali ya chini."

Tags: beiMafutaZanzibarzapaa
TNC

TNC

Next Post

Hofu ya Mungu inavyosaidia kudumisha upendo na amani katika familia

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company