Dar es Salaam. Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, amejiondoa rasmi kwenye mbio za kutetea kiti hicho kwa awamu ya pili.
Dk Tulia alikuwa amechukua fomu za kuwania kutetea nafasi yake na kupitishwa kwenye vikao vya uteuzi vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hata hivyo, amefanya uamuzi wa kujiondoa kwenye mbio hizo.
CCM ilikuwa imempitisha Dk Tulia pamoja na wagombea wengine wawili ambao ni aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu na aliyekuwa mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele.
Kujiondoa kwa Dk Tulia, ambaye pia ni mbunge mteule wa Uyole, kunamaanisha kwamba Zungu na Masele ndio wanabaki kuwania nafasi ya uongozi wa Bunge.
Uchaguzi wa Spika mpya unatarajiwa kufanyika katika kipindi kijacho cha Bunge.