Monday, December 8, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Zubeir achaguliwa tena Spika Baraza la Wawakilishi

by TNC
November 6, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Unguja. Zubeir Ali Maulid amechaguliwa tena kuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa kipindi cha tatu.

Zubeir amechaguliwa leo Alhamisi Novemba 6, 2025 katika mkutano wa kwanza wa Baraza la 11 la Wawakilishi Zanzibar, ambapo hiki kitakuwa kipindi cha tatu tanzu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015.

Spika Zubeir ambaye anatoka kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM), amechaguliwa kwa kupata kura 53 sawa na asilimia 94.6 na kuwabwaga waliokuwa akichuana nao ambao ni Chausiku Khatib Mohamed wa NLD aliyepata kura 3, Naima Salum Hamad wa UDP na Suleiman Ali Khamis wa ADC ambao wote hawakupata kura hata moja.

Kabla ya kupigwa kura, shughuli iliyoongozwa na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Raya Issa Msellem amewapa wagombea wote wanne dakika tano kujieleza na kuomba kura.

Akitangaza matokeo ya kura hizo Raya amesema waliopiga kura ni 68 waliokuwa wamefika ndani ya baraza hilo wakati shughuli ya kuomba na kupiga kura inaanza.

"Kati ya kura zilizopigwa, 12 zimeharibika, kwa hiyo namtangaza Zubeir Ali Maulid amechaguliwa kuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi," amesema Raya.

Baada ya kutangazwa, Zubeir ameapishwa na Katibu wa Baraza la Wawakilishi kushika rasmi madaraka hayo. Akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua kwa kipindi kingine na kuomba ushirikiano ili atimize majukumu yake ipasavyo.

Jukumu la kwanza aliloanza nalo baada ya kuapishwa ni kuwaapisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Wawakilishi, walioapa ni wajumbe 71. Kati ya hao wa majimbo ni 50, viti maalumu 20 na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Mwinyi Talib Haji.

Kutokana na ratiba ya Baraza la Wawakilishi, uchaguzi wa Naibu Spika inatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa Novemba 7, 2025 huku ikisubiriwa kuzinduliwa rasmi kwa Baraza hilo na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.

Tags: AchaguliwaBarazaSpikatenaWawakilishiZubeir
TNC

TNC

Next Post

Cheating and abusive language still undermine national examinations

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company