Thursday, October 30, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Kibatala atia mguu sakata la Niffer

by TNC
October 30, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Polisi Wamshikilia Mfanyabiashara Jenifer Jovin: Wakili Waahidi Msaada wa Kisheria

Dar es Salaam. Wakati Jeshi la Polisi likikiri kumshikilia mfanyabiashara Jenifer Jovin maarufu Niffer kwa tuhuma za uchochezi, Wakili Peter Kibatala ameibuka na kusema kama mfanyabiashara huyo atapelekwa mahakamani atapata msaada wa kisheria.

Kibatala amebainisha hilo leo Jumanne Oktoba 28, 2025 kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiwataja watu wanaondelea kumpigania Niffer.

"Wamepigana sana kwa ajili yako leo, na bado wanaendelea kupigana. Kama Polisi watakupeleka mahakamani Alhamisi, kama wanavyokusudia kufanya, utakuwa na wawakilishi bora kabisa wa kisheria, nchi nzima inakuombea na inakuwazia," amesema.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro alithibitisha kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo kupitia taarifa yake aliyoitoa kwa umma jana Oktoba 27, 2025.

"Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Oktoba 27, 2025 saa 9 mchana eneo la Sinza Kumekucha, limemkamata na linamuhoji Jenifer Bilikwiza Jovin miaka 26 mkazi Masaki Peninsula Kinondoni," taarifa ya polisi ilieleza.

Kulingana na taarifa za jeshi hilo, Niffer anashikiliwa kwa tuhuma za kuhamasisha vurugu na kuharibu miundombinu katika maeneo mbalimbali jijini hasa siku za kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.

Kamanda Muliro katika taarifa hiyo, alieleza kuwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuzingatiwa dhidi ya mtuhumiwa.

Kabla ya taarifa hiyo ya Polisi, zilisambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mfanyabiashara huyo ametekwa na watu wasiojulikana katika duka lake Sinza jijini Dar es Salaam.

Uchunguzi wa TNC umebaini kuwa duka lake la Sinza Kumekuwa, Dar es Salaam limefungwa huku baadhi ya makabati ya kuweka bidhaa yakiwa nje.

Mbali na dukani hapo hata katika saluni yake iliyopo Mwananyamala nayo imepigwa kufuli kuashiria hakuna shughuli zozote zinazoendelea mahali hapo.

Tags: AtiaKibatalamguuNifferSakata
TNC

TNC

Next Post

Othman aibua tuhuma kuhusu uchaguzi, taasisi ya uchaguzi inatoa onyo

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company