Uchaguzi Mkuu Tanzania 2025: Upigaji Kura Unaendelea Kwa Amani Nchini
Dar es Salaam/Mikoani – Shughuli ya upigaji kura katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania kuwachagua madiwani, wabunge na Rais inaendelea huku hali ya utulivu ikitawala.
Kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), vituo vilipaswa kufunguliwa saa 1:00 asubuhi na vitafungwa saa 10:00 jioni ya leo Jumatano, Oktoba 29, 2025.
Hata hivyo, baadhi ya maeneo hadi saa 2 asubuhi vituo vilikuwa havijafunguliwa na maeneo mengine vilifunguliwa na upigaji kura unaendelea.
Watanzania milioni 37.6 ndiyo waliandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao ndiyo wanaoshiriki shughuli hiyo ya upigaji kura.
Wananchi katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Temeke, Nyambwera, Manyimbwi, Chatembo, Kata ya Mwandege Mkuranga, Kikwajuni Mjini Magharibi, na Haile Selassie Malindi Unguja wamejitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huu mkuu.
Hali ya utulivu na nidhamu inaendelea kuonekana katika vituo mbalimbali vya upigaji kura ambapo wananchi wamepata fursa ya kutekeleza haki yao ya kiraia.
Endelea kufuatilia TNC kwa habari zaidi.