Thursday, October 30, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Jinsi AI ilivyosaidia kampuni ya simu kupunguza matukio ya udanganyifu

by TNC
October 28, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dar es Salaam. Airtel Tanzania imefanikiwa kupunguza matukio ya jaribio la udanganyifu kwa asilimia 12.5 kwa robo mbili mfululizo, ikilinganishwa na watoa huduma wengine wa mawasiliano nchini.

Mafanikio hayo yametokana na matumizi ya mfumo wa Akili Bandia (AI) wa kugundua spam na kutoa tahadhari za udanganyifu kwa wateja wake.

Kulingana na ripoti ya takwimu za mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka huu, Airtel Tanzania imepunguza matukio ya jaribio la udanganyifu kutoka 2,595 yaliyorekodiwa Juni hadi 1,559, sawa na punguzo la 1,036.

Hata hivyo, ripoti hiyo inaonesha kuwa kwa jumla, majaribio ya udanganyifu kwa kampuni zote tano yamepungua kwa asilimia 10, kutoka 13,837 hadi 12,475, huku mikoa ya Rukwa na Morogoro ikiongoza kwa idadi kubwa ya matukio ya majaribio ya udanganyifu.

Ripoti iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabir Bakari, inaonesha kuwa mikoa ya Rukwa na Morogoro imerekodi idadi kubwa ya majaribio ya udanganyifu, ikifuatiwa na Dar es Salaam, Mbeya na Kilimanjaro ambazo zimeshika nafasi ya tatu, nne na tano mtawalia.

Mikoa ya Kaskazini Unguja, Kusini Unguja na Kaskazini Pemba imerekodi idadi ya chini zaidi ya majaribio ya udanganyifu.

"Kwa ujumla, utendaji wa robo hii unathibitisha kasi kubwa kuelekea Tanzania iliyounganishwa, salama, jumuishi na yenye nguvu za kidijitali. TCRA inabaki imejitolea kuwezesha mazingira yanayohimiza uwekezaji kwenye miundombinu, uvumbuzi na ukuaji endelevu wa mfumo wa mawasiliano kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa na dira ya uchumi wa kidijitali," inasomeka sehemu ya ripoti hiyo.

Mwaka huu, Airtel Tanzania imezindua Spam Alert – Kataa Matapeli, mfumo wa kwanza barani Afrika wa Akili Bandia (AI) unaogundua spam na kutoa tahadhari za udanganyifu.

Huduma hiyo inatumia AI kubaini ujumbe unaoshukiwa na kutoa tahadhari kwa watumiaji kwa wakati halisi ili kuwasaidia kuepuka udanganyifu.

Kifaa hicho cha ubunifu kilizinduliwa kama sehemu ya kampeni ya kitaifa ya #SITAPELIKI ya kupambana na udanganyifu na kuunganisha Airtel Tanzania na juhudi za Serikali za kuongeza usalama wa watumiaji wa simu, kilichozinduliwa Februari mwaka huu.

Ripoti ya TCRA inaonesha kuwa Vodacom inaongoza kukumbwa na majaribio ya udanganyifu kwa asilimia 31.9, ikifuatiwa na Yas kwa asilimia 19.7, Halotel asilimia 18.2 na TTCL asilimia 17.8.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masuala ya Udhibiti wa Airtel, Beatrice Singano, amesema matokeo ya kampeni ya Airtel Kataa Matapeli yanaonekana wazi, ambapo majaribio ya udanganyifu yamepungua kutoka asilimia 19 hadi 12 kufikia Septemba.

Singano amesema huduma ya Airtel Spam Alert, elimu kwa wateja na hatua madhubuti za usalama zimeleta mabadiliko makubwa katika kukabiliana na majaribio ya udanganyifu.

Ameongeza kuwa kampuni itaendelea kuwalinda wateja wake na kuhakikisha mazingira salama ya kidijitali yanaendelea kuwepo muda wote.

Tags: ilivyosaidiaJinsiKampuniKupunguzaMatukiosimuUdanganyifu
TNC

TNC

Next Post

Maktaba na usomaji vinakufa, tuamke kuokoa hali

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company