Thursday, October 30, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Sh21.9 bilioni kuibadilisha Mpanda

by TNC
October 26, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Wananchi wa Mpanda Watarajia Mabadiliko Makubwa ya Kiuchumi kupitia Mradi wa Tactic

Katavi. Wananchi wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, wanatarajia kunufaika na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kupitia utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (Tactic).

Mradi huo utagharimu Sh21.9 bilioni na utatekelezwa chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.

Hayo yameelezwa Jumapili, Oktoba 26, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa miundombinu kupitia mradi huo.

Mrindoko amesema mradi huo utakuwa chachu ya maendeleo kwa kuboresha miundombinu ya usafiri, mazingira ya biashara na kuongeza mapato ya halmashauri.

Amemtaka mkandarasi M/s Chongqing International Construction Corporation (CICO) kuhakikisha kazi inafanyika kwa ubora, kasi na kukamilika kwa wakati, huku akiwataka watendaji wa Manispaa ya Mpanda na Wakala wa Barabara Vijijini (Tarura) kushirikiana katika usimamizi wa mradi huo.

Kupitia mkataba huo, CICO itajenga barabara za lami zenye urefu wa kilomita 8.4, jengo la usimamizi wa mradi na ununuzi wa magari manne ya kufuatilia utekelezaji wa kazi.

Mradi unatarajiwa kuanza rasmi Novemba Mosi mwaka huu na kukamilika ndani ya miezi 15.

Kwa upande wake, Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Tactic kutoka Tarura, Emmanuel Manyanga amesema lengo la mradi ni kuboresha miundombinu ya miji 45 nchini na kuzijengea uwezo halmashauri katika usimamizi wa maendeleo ya miji na ukusanyaji mapato.

Manyanga amesema mpango huo unaolenga kuboresha usimamizi wa ukuaji wa miji, utaiwezesha Manispaa ya Mpanda kuvutia wawekezaji, kupanua shughuli za kiuchumi na kuimarisha ustawi wa wananchi.

"Tunataka kuona miji yetu ikitoa huduma bora na yenye tija kwa wananchi. Huu ni mwanzo wa mageuzi makubwa ya maendeleo katika Mkoa wa Katavi," amesema Manyanga.

Tags: BilionikuibadilishaMpandaSh21.9
TNC

TNC

Next Post

Wagombea urais watakavyopishana kufunga kampeni, kupiga kura

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company