Thursday, October 30, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Ofisi ya Mufti yaeleza sababu za kutofunga madrasa siku ya uchaguzi

by TNC
October 26, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Unguja – Ofisi ya Mufti Zanzibar imeeleza sababu za kutofunga madrasa wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu ili kuondosha hofu na kujenga taharuki kwa wananchi kwamba hakuna amani.

Ofisi hiyo pia imewatahadharisha waandishi wa habari kuzingatia weledi na kuacha kuandika habari zitakazoleta taharuki na kusababisha mgawanyiko miongoni mwa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jumapili Oktoba 26, 2025, Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti, Sheikh Khalid Ali Mfaume amesema hawakuona sababu ya kufunga madrasa Oktoba 29, 2025 siku ya uchaguzi kwa sababu kufanya hivyo ni kuleta wasiwasi na taharuki kwa wananchi.

"Hatukufunga kwa sababu bado kuna amani, sasa tukifunga madrasa kwa sababu ya uchaguzi tunaongeza taharuki na kuonesha kana kwamba hakuna amani, bado tuna amani hali ni shwari," amesema.

Sheikh Mfaume amesema kuna taarifa potofu zinazoshwa mitandaoni baada ya taarifa kutolewa za kufungwa kwa shule.

"Kufungwa kwa shule kuna sababu. Baadhi zitatumika kama vituo vya kupigia kura na si vinginevyo, sisi madrasa zetu hazitumiki kama vituo vya kupigia kura, kwa nini tuzifunge? Hivyo natamka kwamba madrasa hazitafungwa, tunaendelea na madarasa yetu kama kawaida," alisema.

Sheikh Mfaume amesema ofisi ya Mufti inasisitiza kuendeleza amani na utulivu wakati wa uchaguzi kwa kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi mkuu.

Ofisi ya Mufti imewatahadharisha waandishi wa habari kutotoa taarifa za taharuki ambazo hazina ukweli kuelekea Oktoba 29, 2025, siku ambayo Watanzania watapiga kura kuwachagua viongozi wao watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mkuu wa Divisheni ya Fatwa na Utatuzi wa Migogoro, Sheikh Shaaban Al Batashi amesema taarifa za upotoshaji zinasababisha hofu, wasiwasi na kuleta mgawanyiko miongoni mwa wanajamii.

"Taarifa hizi zinaathiri mtazamo wa wananchi na kuunda mitazamo isiyo sahihi na kutengeneza chuki," amesema.

Pia, amesema katika kutoa taarifa za upendeleo na kumbeba mtu fulani zinaweza kuchochea chuki miongoni mwa wagombea na wafuasi wao na kuwavunja moyo wananchi wakaacha kujitokeza kwenda kupiga kura, na baadaye kufanya shughuli zao za kijamii ikiwamo kujitafutia mahitaji yao ya kila siku.

Sheikh Masoud Ahmada amesema ni wajibu kuchuja mambo badala ya kuandika kila kitu.

"Ukiandika uongo unasababisha uovu, ukweli ndio utakuweka huru na kuokoa katika hatari, ni vyema kuchukua tahadhari na kuwa wakweli," amesema.

Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrissa Kitwana amewaondolea hofu wananchi kwamba hakutakuwa na changamoto ya usalama hivyo wasifunge biashara zao kisa uchaguzi.

Tags: kutofungamadrasaMuftiOfisiSababuSikuuchaguziyaeleza
TNC

TNC

Next Post

Kama unaangalia video Instagram ghafla ikakupotea fanya hivi kuiona tena

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company