Thursday, October 30, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

TPDC yatumia Sh3.4 bilioni kuboresha miradi ya kijamii Mtwara, Lindi

by TNC
October 25, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

TPDC Yatumia Sh3.4 Bilioni Katika Miradi ya Maendeleo Mtwara na Lindi

Dar es Salaam – Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetumia jumla ya shilingi bilioni 3.4 katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii zinazozunguka maeneo yenye shughuli za mafuta na gesi asilia mikoa ya Mtwara na Lindi.

Utekelezaji wa miradi hiyo ni sehemu ya dhamira ya shirika hilo la kuhakikisha wananchi wananufaika moja kwa moja na rasilimali za mafuta na gesi.

Meneja Mawasiliano wa TPDC, Marie Msellemu, amesema miradi hiyo imetekelezwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 na 2024/25, ikijikita katika sekta za afya, elimu, maji, usalama na miundombinu.

"Tunataka wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya miradi ya mafuta na gesi wawe miongoni mwa wanufaika wakuu wa shughuli hizi. Ndiyo maana TPDC imewekeza kwenye miradi inayogusa maisha yao moja kwa moja," amesema Msellemu.

Miradi Mkoa wa Mtwara

Kwa Mkoa wa Mtwara, TPDC imejenga kituo cha afya Msimbati kwa shilingi milioni 759.9, kituo cha polisi Msimbati kwa shilingi milioni 186.2, pamoja na uwekaji wa taa za barabarani katika vijiji vya Mngoji na Msimbati kwa shilingi milioni 498.21.

Miradi mingine inayoendelea ni pamoja na mradi wa maji kijiji cha Mngoji kwa shilingi milioni 47.7, mradi wa maji kutoka kijiji cha Mayaya hadi Mahiva kwa shilingi milioni 38.8, na ujenzi wa kituo cha afya Mtendachi kwa shilingi milioni 38.84.

TPDC pia inatekeleza ujenzi wa kituo cha afya Nanyamba kwa shilingi milioni 400.

Miradi Mkoa wa Lindi

Kwa Mkoa wa Lindi, TPDC imetekeleza ujenzi wa Shule ya Msingi Likongo kwa shilingi bilioni 1.3, ujenzi wa madarasa matatu katika Shule za Msingi Marendego na Kilwa Masoko kwa shilingi milioni 72, na ujenzi wa madarasa katika eneo la Mbwemkuru kwa shilingi milioni 20.

Mradi wa maji Kilangala B wenye thamani ya shilingi milioni 50 umekamilika na unafanya kazi.

Msellemu ameongeza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unaonyesha dhamira ya TPDC kuimarisha mahusiano na jamii sambamba na kuchochea maendeleo endelevu katika maeneo yanayohusiana na sekta ya mafuta na gesi nchini.

Jamii Inashukuru

Ofisa Mtendaji Kata ya Somanga wilayani Kilwa, Salum Kumbora, amesema jamii inanufaika kutokana na miradi mbalimbali inayotekelezwa na TPDC.

"Tunawapongeza TPDC kwa namna ambavyo wanaishika jamii mkono, wametujengea shule kuwasaidia wanafunzi, wanafunzi na walimu sasa wanasoma na kukaa katika mazingira mazuri, pia tumepata madawati. Hii imetusaidia wanafunzi kupata hamasa ya kuhudhuria shule bila kukosa kutokana na mazingira kuwa mazuri," amesema.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Marendego, Shaban Nasoro, amesema walikuwa na uhaba mkubwa wa madarasa na sasa kukamilika kwa ujenzi wa madarasa matatu kumeondoa adha waliyokuwa wanapata kwa wanafunzi kukaa wengi kwenye darasa moja.

Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji Marendego, Said Yusuph, amesema kimbunga Hidaya kilisababisha madarasa mengi katika kijiji hicho kuezuliwa na hivyo msaada huo umekuwa na tija kwa wakazi.

"Tunaahidi kutokana na mradi huu kukamilika kwa wakati na wanafunzi wetu wanasoma, kwa uhakika tutatunza mradi huu uwe endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Tutaweka mlinzi ili miradi hii isiharibiwe na watu wasiopenda maendeleo," amesema.

Tags: BilioniKijamiikuboreshaLindimiradiMtwaraSh3.4TPDCyatumia
TNC

TNC

Next Post

Key Police witness concludes evidence in opposition politician Tundu Lissu treason trial

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company