Huduma Mpya ya Tiba ya Urejeshaji: Mbadala wa Upasuaji wa Plastiki
Dar es Salaam. Huduma mpya ya tiba ya urejeshaji inayotumia seli shina za mwili wa binadamu inaanza kubadilisha sekta ya afya na urembo, kwa kuwa mbadala wa upasuaji wa plastiki.
Tiba hii ya kisasa, inayogharimu kati ya Dola 200 hadi 300 za Marekani kwa kila kikao, husaidia mwili kujitibu kwa kutumia seli zake asilia bila kuathiri maungo.
Manufaa ya Tiba ya Urejeshaji:
– Kurejeshwa ngozi iliyochoka
– Kuota nywele mpya
– Kupunguza mikunjo na kasi ya kuzeeka
– Kujenga misuli
– Kuponya vidonda
– Kupunguza maumivu ya viungo
Tofauti Muhimu na Upasuaji wa Plastiki:
– Haina majeraha
– Muda mfupi wa kupona
– Matokeo ya kudumu
– Gharama nafuu
– Usalama zaidi kwa mwili
Tiba ya urejeshaji inaonyesha matumaini makubwa katika sekta ya afya, na inatarajiwa kuenea kwa kasi nchini na bara Afrika.