AJALI YA KANISA ETHIOPIA: WATU 30 WAFARIKI, ZAIDI YA 200 WAJERUHIWA
Ajali ya kuuguza moyo imetokea nchini Ethiopia, ambapo jengo la kanisa la Menjar Shenkora Arerti Mariam limeporomoka na kusababisha kifo cha watu 30 na kujeruhia zaidi ya 200.
Tukio hili lilifanyika Jumatano, Oktoba 1, 2025, katika eneo la Amhara, wakati waumini walikuwa wamekusanyika kwa sherehe ya kumuenzi Mtakatifu Maria.
Serikali ametoa pole kwa familia za waathirika na kusisitiza umuhimu wa usalama wakati wa ujenzi wa majengo.
Mtaalamu wa afya amesema kuwa miongoni mwa waathirika wako watoto na wazee, na hatari ya idadi ya vifo kuongezeka bado ipo. Baadhi ya watu bado wamekwama chini ya vifusi na timu ya uokoaji inaendelea na juhudi.
Mashuhuda wameeleza kuwa waumini wengi walikuwa wamepanda sehemu ya juu ya kanisa wakitazama ujenzi, mara tu kabla ya kuanza sherehe.
Majeraha wamepelekwa hospitali kubwa ya Addis Ababa kwa matibabu ya haraka.