Mgombea wa Chama cha Makini Aahidi Mabadiliko Makubwa kwa Wakazi wa Mbalizi
Mbeya, Septemba 27, 2025 – Mgombea urais, Coaster Kibonde, ametumia asili yake ya Mbalizi kuwaomba wananchi wa eneo hilo, akiwaahidi mabadiliko ya msingi katika sekta za kilimo, elimu na afya.
Akihutubia mkutano wa kampeni, Kibonde alisema kuzaliwa kwake Mbalizi ni fursa ya kipekee kwa wakazi kumuunga mkono. Ameainisha sera muhimu zikiwamo:
Elimu:
– Elimu bure kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu
– Masomo yatalenga ujuzi wa soko la ajira
– Kuwasomesha wanafunzi hata nje ya nchi
Kilimo:
– Vijana watapatiwa ekari tano zenye hati miliki
– Wakulima watapatiwa matrekta
– Soko huria la kuuza mazao
Afya:
– Ujenga wa hospitali za kata zenye vifaa na wataalamu
– Huduma ya ‘Makini Care’ itakayotolewa bure
Kibonde ameahidi pia kuongeza mishahara ya chini hadi Sh600,000 na kutoa mikopo isiyo na riba kwa wafanyabiashara wadogo.
“Falsafa yangu ni kuwatumikia wananchi. Naomba kura zenu Oktoba 29, ili niunganishe wilaya kwa wilaya kwa kiwango cha lami,” alisema.