Taarifa Kubwa: Maofisa 4 wa Polisi Washtakiwa kwa Wizi wa Pikipiki Moshi
Moshi – Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imeahirisha kesi ya maofisa 4 wa polisi walioshtakiwa kwa wizi wa pikipiki kwa kutumia silaha.
Maofisa hao wanahusika katika kesi ya jinai namba 20614/2025, ambao wanashitakiwa kwa kubeba silaha na kuiba pikipiki aina ya Sinoray yenye namba za usajili MC 406 ERU, iliyokuwa ya mmiliki Ramadhan Singe.
Washtakiwa ni:
– G.2478 Ramadhan Jumanne
– F.7340 Goodluck Richard
– G.654 Zakayo Sanga
– Victor Shelukindo
Kesi hiyo imepewa muda mpaka Septemba 17, 2025, ili kuwezesha ukamilishaji wa uchunguzi. Kwa mujibu wa sheria, washtakiwa hawatapewa dhamana na wataendelea kuhifadhiwa gerezani.
Jambo la kushangaza ni kuwa kesi hii inatokea baada ya mwendesha bodaboda Deogratius Shirima (35) kutoweka Julai 21, 2025, ambapo pikipiki yake ilidaiwa kuwa ndani ya kambi ya polisi.
Uchunguzi unaendelea na maafisa wa juu kutoka Dodoma wameanza kuchunguza tukio hili.