Mgogoro Mkubwa Umeibuka Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisis ya Konde
Mbeya – Mgogoro mkubwa umeibuka katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKT) Dayosisi ya Konde Usharika wa Forest jijini Mbeya, baada ya waumini kupinga uamuzi wa kusimamishwa kwa viongozi wao na Kwaya Kuu.
Novemba mwaka jana, 2024, kanisa hilo lilipokea waraka kutoka jimboni unaoangazia kupunguza idadi ya Kwaya ndani ya usharika huo hadi tatu. Kwaya zilizotajwa kupunguzwa ni Kwaya Safina na Hosiana, huku uongozi wa kanisa ukitaka Kwaya Kuu kufutwa na wanakwaya kujisajili upya.
Awali, usharika huo una Kwaya tano ambazo ni Kwaya Kuu Forest, Kwaya Uinjilisti, Kwaya Hosiana, Kwaya Safina, Kwaya Vijana na Kwaya Uwaki.
Waumini wamesikitishwa sana na uamuzi huo, wakidai kuwa Kwaya Kuu ina historia ya miaka 45 tangu kuanzishwa. Katibu wa Kwaya Kuu, Julius Mwaikusi ameeleza kuwa barua iliyotoka Dayosisi ilitoa maelekezo ya kupunguza Kwaya, jambo ambalo limesababisha mgogoro mkubwa.
Viongozi wanaohusika wamesema kuwa sababu ya mgogoro ni ununuzi wa gari na uhasibu wa rasilimali za Kwaya. Makamu Katibu wa Kwaya Kuu, Rehema Ibanje ameishia kusema kuwa wanataka kuhifadhi mali zao na kupinga uamuzi wa kubadilisha uongozi.
Mkuu wa Jimbo la kanisa, Lusajano Sanga ameeleza kuwa bado hajapokea taarifa kamili juu ya mgogoro huo na anasubiri maelezo ya kina kutoka kwa mchungaji wa kanisa.
Hali hii imeikumba kanisa katika hali ya kutofautiana, na waumini wanataka utulivu na ufafanuzi wa haraka juu ya mgogoro huu.