Elon Musk Apoteza Bilioni 12 Baada ya Mapato ya Tesla Kushuka
Bilionea duniani Elon Musk amepoteza zaidi ya dola bilioni 12 ndani ya saa 24, baada ya kampuni yake ya magari ya umeme kushuka kwa mapato ya kihistoria.
Ripoti ya fedha ya robo ya pili ya mwaka 2025 imeonesha kuwa Tesla imepata mapato ya bilioni 19.6, punguzo la asilimia 15 ikilinganishwa na mwaka jana. Hiki ni kushuka cha kwanza kwa kampuni tangu mwaka 2020.
Kushuka huku kumechangia kupungua kwa thamani ya hisa za Tesla kwa asilimia 12 kwenye soko, ambapo utajiri wa Musk umeshuka hadi bilioni 193.
Musk anakabiliwa na changamoto za soko, ikijumuisha ushindani mkali kutoka kwa wazalishaji wa magari ya umeme, hasa kutoka China.
Wachambuzi wa uchumi wanasema kushuka kwa mapato kunaweza kuashiria mabadiliko katika mahitaji ya soko la magari ya umeme.
Hata hivyo, Musk amesema Tesla itaendelea kuwekeza kwenye teknolojia mpya na kupanua uzalishaji wake duniani, hasa katika masoko ya Asia na Afrika.
“Tunaamini njia ya kuelekea katika ufanisi wa muda mrefu bado ipo wazi, na tutazidi kuwekeza kwenye ubunifu,” amesema Musk.
Tangu mwaka 2020, Tesla imeona mabadiliko makubwa ya mapato, kufikia kilele cha bilioni 81.5 mwaka 2022, lakini sasa inakumbwa na changamoto za kushuka kwa mapato.