Mtu Ajinyonga Arusha Baada ya Kudaiwa Kudhulumiwa Mbuzi
Arusha – Mkazi wa Kijiji cha Nambere, Wilaya ya Arumeru Joseph Melau, aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 60 na 65, amefariki dunia kwa kujinyonga nyumbani kwake baada ya mgogoro wa mbuzi.
Taarifa za awali zinaonesha kuwa Melau alizinunua mbuzi mbili kutoka kwa kaka wake na kuziweka muda katika banda la mifugo, akisubiri kukamilisha ujenzi wake binafsi. Hata hivyo, siku alipokuwa anatakiwa kuwachukua, alinyimwa, jambo linalodaiwa kumsababishia msongo mkubwa wa mawazo.
Mtoto wake, Wilson Joseph, alisema baba yake alirudi nyumbani Juni 6, 2025 akiwa na hasira sana, akieleza kuwa amepigwa na ndugu zake na kunyimwa mbuzi wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha kifo hiki. “Upelelezi bado unaendelea kuhusu mazingira ya tukio hili,” amesema.
Jirani ya marehemu, Lucas Kabaha, ameeleza kuwa tukio hilo labda lilitokana na ukosefu wa mtu wa karibu na Melau, ambaye alikuwa anaishi peke yake.
Polisi inaendelea na uchunguzi wa kina ili kubainisha hala halisi ya kifo hiki.