Makala ya Maudhui: Mtazamo wa Vita ya Kisiasa Tanzania – “No Reforms, No Election” dhidi ya “Oktoba Tunatiki”
Taifa limevikwa na mkumbo wa kauli mbiu ya kisiasa. Upande mmoja umeanza kuchafua mitandao kwa kuandika maoni ya “No Reforms, No Election”, ikitaka kubadilisha mfumo wa uchaguzi wa nchi.
Kauli mbiu hii ya “No Reforms, No Election” inazungushwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), lengo lake kuzidisha shinikizo kwa serikali na Tume ya Uchaguzi, kusisitiza kwamba bila mabadiliko ya Katiba, hakutakuwa na uchaguzi mwaka 2025.
Mtandao umejaa mashindano ya maoni, ambapo kila posti ya kiongozi imekuwa sehemu ya vita ya kisiasa. Upande mmoja unasukuma slogan ya “No Reforms, No Election” wakati mwingine CCM inajibu na “Oktoba Tunatiki”, lengo lake kumchagua Rais Samia Suluhu Hassan.
Uchambuzi wa kimaudhui unaonesha kuwa haya ni matokeo ya wasiwasi wa kisiasa, ambapo posti nyingi zinatumia akaunti bandia ili kuonesha msimamo. Mbinu hizi za propaganda na PsyOps zinaashiria kupanika kisiasa, ambapo vyama vya siasa havijajikita kwenye mazungumzo ya kiufundi.
Dalili za hali hii ni kusababisha maudhui ya mitandao kujazwa na mapambano ya kisiasa badala ya mazungumzo ya kibunifu. Hii inaonesha hitaji la kuboresha mbinu za mazungumzo ya kisiasa ili kuleta manufaa kwa taifa.
Jambo la msingi ni kuwa siasa inabadilika na inahitaji mbinu za kujadili ambazo zinajenga, si kubomoa. Vyama vya siasa wanahitaji kurejea kwenye mazungumzo ya kitaaluma na kuacha vita za kimtandao.