Halotel Lazindua Huduma Mpya ya Huduma Kwa Wateja ‘Miss Halo’ Kurahisisha Mawasiliano
Kampuni ya Halotel imezindua huduma mpya ya wateja inayoitwa ‘Miss Halo’ ambayo itawezesha wateja kuwasiliana na kampuni kwa urahisi zaidi na haraka.
Huduma hii itakuwa ya digitali na kutumia mitandao mbalimbali, ikiwapo kwa namba 0620100100, ambapo wateja wataweza kupata msaada wa moja kwa moja, kuangalia salio na kununua vifurushi mbalimbali.
Abdallah Salum, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara, alisema huduma hii ni manufaa kwa wateja kwani itatoa upatanishi wa haraka na kuondoa changamoto za mawasiliano.
“Dunia inaenda kidigitali na sisi lazima twende na teknolojia ya kisasa ili kupunguza masuala ya utapeli mitandaoni,” alisema Salum.
Shabani Said, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, alisisitiza umuhimu wa ubunifu katika sekta ya mawasiliano, akidokeza kuwa ‘Miss Halo’ ni njia ya kuhakikisha wateja wanapata msaada wa haraka na wa kuaminika.
Huduma hii itakuwa rahisi kwa watumiaji kwani imeandaliwa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza, hivyo kurahisisha matumizi.
Roxana Kadio, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, alisema kampuni inaendelea kuimarisha huduma zake ili kuboresha maisha ya watumiaji wake.
Halotel inatarajiwa huduma hii itakuwa jambo la muhimu sana kwa wateja wake na kuboresha ufanisi wa mawasiliano.