TAHARUKI: WANAUME WAPO HATARINI ZAIDI KUFA KWA MAGONJWA YASIYO AMBUKIZA
Ripoti mpya ya Shirika la Afya Duniani inaonesha wanaume wapo hatarini zaidi kufa kwa magonjwa yasiyo ambukiza (NCDs), ikilinganishwa na wanawake. Takwimu zinaonesha kuwa vifo vitokanavyo na magonjwa haya vimeongezeka kutoka asilimia 34 mwaka 2019 mpaka 38.8 mwaka 2021.
Takwimu za mfumo wa taarifa za uendeshaji wa huduma za afya zinaonesha ongezeko la wagonjwa wa NCDs kutoka 2,626,107 mwaka 2019 hadi 3,140,067 mwaka 2021, sawa na ongezeko la wagonjwa 513,960 au asilimia 20.
Kwa kila wanaume 100,000 wa Tanzania, uwezekano wa kufa kwa magonjwa yasiyo ambukiza ni 557 ikilinganishwa na 498 kwa wanawake. Hatari hii inachangiwa na mambo mbalimbali:
• Vyakula visivyofaa
• Kutofanya mazoezi
• Uzito kupita kiasi
• Vitambi
• Presha
• Kisukari
• Matumizi ya pombe
• Uvutaji wa sigara
Magonjwa ya mfumo wa upumuaji yaliongoza kwa vifo, ikifuatiwa na malaria, kifua kikuu, Ukimwi, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.
Wataalamu wanaishiya wanaume waangalie afya zao mapema, kufanya vipimo mara kwa mara na kubadilisha mtindo wa maisha ili kupunguza hatari ya magonjwa haya.