Rais Samia Aagiza Mapitio ya Fidia kwa Wananchi Walioathiriwa na Wanyamapori
Lushoto, Tanga – Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo la kufanya mapitio ya kanuni za fidia kwa wananchi wanaoathiriwa na wanyamapori, kwa lengo la kuhakikisha fidia zinatolewa kwa kiwango kinachostahili.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Lushoto, Rais Samia ameeleza kuwa agizo hilo linalenga kulinda wananchi dhidi ya madhara ya wanyama waharibifu, hasa tembo wanaoharibu mazao ya mahindi.
Ameagiza Waziri wa Maliasili na Utalii kuchunguza uwezekano wa kubadilisha kanuni za fidia ili ziweze kuwalinda wananchi. “Namwagiza Waziri aangalie uwezekano wa kufanya mapitio ya kanuni za fidia kwa wale wanaoingiliwa kwenye mashamba yao,” alisema Rais.
Sambamba na hilo, Rais ametathmini juhudi za serikali katika kulinda wananchi, ikijumuisha kuongeza askari wa wanyamapori na kutumia teknolojia ya drone.
Katika hatua nyingine muhimu, Rais Samia ameahirisha kuwa Machi 6 zabuni itafunguliwa kwa ujenzi wa barabara ya Soni-Bumbuli, yenye urefu wa kilomita 31, ili kuboresha mawasiliano.
Aidha, ameisifu wilaya ya Lushoto kwa utunzaji wa mazingira, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza mazingira salama na yenye hewa safi.
Ziara hiyo pia iliangazia mradi wa Bwawa la Umwagiliaji la Mkomazi, mradi wa Sh18 bilioni utakaochangia maendeleo ya kata saba na kuhudumia wananchi zaidi ya 20,000.
Rais Samia ameihimiza Lushoto kuendelea na juhudi za kuboresha mazingira na huduma kwa wananchi, akizisisiitiza umuhimu wa matumizi bora ya rasilimali.