Onyo la Hali Mbaya ya Hewa: Mikoa Mitano Itaathirika na Upepo Mkali
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa onyo la hali mbaya ya hewa kwa siku tano, ikitabiri upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi ya mita mbili.
Mikoa inayohusika itajumuisha ukanda wa pwani wa kaskazini, ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam, Tanga, Pwani, na visiwa vya Mafia, Pemba na Unguja. Hali hii itaanza Ijumaa Februari 21, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa ya TMA, Februari 22, 2025 utakuwa na athari kubwa zaidi katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara, pamoja na visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.
Athari zinazotarajiwa ni za kati ya wastani, na zinaweza kuathiri shughuli mbalimbali za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini. Wananchi wa mikoa husika wanapaswa kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari zinazohitajika.
TMA inawasihi wananchi kufuata maelekezo ya usalama na kuepuka maeneo hatarishi wakati wa hali hii ya hewa mbaya.