URAIBU WA SIMU: ATHARI KUBWA ZA MATUMIZI YASIYOPIMIKA YA MITANDAO
Dar es Salaam – Matumizi ya simu za mkononi duniani yanaongezeka kwa kasi kubwa, na wasomi wa afya ya akili wanaeleza kuwa matumizi haya yanaweza kuleta athari kuu kwa afya ya binadamu.
Teknolojia ya sasa imeifanya simu kuwa zana kubwa zaidi ya mawasiliano, ambapo ulimwengu mzima unaweza kufikiwa kwa kubonyeza kidogo tu. Hata hivyo, matumizi ya ziada ya mitandao ya kijamii yanasababisha changamoto kubwa za kiafya.
Wataalamu wa saikolojia wamebaini kuwa matumizi ya ziada ya mitandao yanaweza:
• Kupunguza uwezo wa mawasiliano ya mtu uso kwa uso
• Kuathiri uhusiano wa kibinadamu
• Kupunguza ufanisi wa kazi
• Kubadilisha tabia ya jamii
Mtaalam wa saikolojia ameeleza kuwa matumizi ya mitandao yanazalisha kemikali ya dopamine ambayo inaweza kusababisha uraibu. Hii kemikali hufanya mtu ajisikie vizuri, hivyo anayetumia mitandao kwa muda mrefu anaweza kupatwa na tabia hiyo.
Namna ya kujikinga:
1. Tambua kuwa una tatizo
2. Weka simu mbali mara baada ya kuamka
3. Usichezee na simu wakati wa familia na marafiki
4. Punguza muda wa kuangalia mitandao
Wataalamu wanatahadharisha kuwa endapo hali hii itaendelea, inaweza kuleta athari kubwa kwa jamii katika miaka ijayo.