Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Inatekeleza Mifumo Mitano Muhimu ya Kidijitali
Arusha – Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeanza hatua muhimu katika kuboresha teknolojia ya taifa kwa kutekeleza mifumo mitano muhimu ya kidijitali ambayo itakuwa chachu ya maendeleo ya taifa.
Mifumo hii inajumuisha:
– Mfumo wa ubadilishanaji taarifa
– Mfumo wa utambuzi kidijitali
– Jamii Namba
– Mfumo wa utambuzi wa wateja
– Mfumo wa malipo ya kidijitali
– Mfumo wa usajili wa wadau wa utafiti
Lengo kuu ni kuharakisha ukuaji wa uchumi wa kidijitali na kuboresha huduma za kimtandao kwa wananchi.
Aidha, Wizara imeanza mradi wa ujenzi wa Chuo Mahiri cha Tehama mjini Dodoma, mradi utakaogharimu fedha za kimarekani zaidi ya milioni 175.8.
Wizara pia inahakikisha maendeleo ya watumishi wake kwa kuwapatia mafunzo ya shahada ya uzamili nchini na nje ya nchi, pamoja na kuhakikisha usalama wa taarifa za kitaifa.
Kipaumbele kikubwa ni kuwa watumishi wote waendelee kufanya kazi kwa bidii, kuwa na siri ya kazi na kuhifadhi maslahi ya taifa.