MGOGORO WA ARDHI HANDENI: HALMASHAURI YAFUNGA OFISI KWA SIKU 14
Halmashauri ya Mji wa Handeni imeamua kufunga ofisi ya ardhi kwa siku 14 kulingana na mgogoro unaoendelea katika eneo la Kitalu A, Kata ya Kwenjugo.
Mgogoro huu unatokana na halmashauri kuchukua viwanja vya wananchi kwa makubaliano ya kuwalipa fidia, ambapo wananchi hawakufidiwa. Badala yake, viwanja vimegawiwa kwa watu wengine.
Viwanja 580 vimehusika katika mgogoro huu, ambapo wamiliki wa awali hawakukamilisha malipo ya upimaji ya shilingi 120,000 kwa kila kiwanja.
Mwenyekiti wa Halmashauri, Mussa Mkombati, amesema kuwa ofisi ya ardhi itafungwa mpaka Waziri wa Ardhi atakapofika kutatua mgogoro huu. Hatua hii imetokana na changamoto za muda mrefu ambazo hazija kamilishwa.
Uamuzi huu umefikiwa baada ya tathmini ya mapendekezo ya viongozi mbalimbali, ikiwemo ofisi ya mkuu wa wilaya na chama cha CCM.
Halmashauri inasistiza kuwa hatua hii itasaidia kuhakikisha mgogoro unatatuliwa kwa njia ya kiutalaamu na kulinda usalama wa wananchi.