Takukuru Yarejeshi Sh13.7 Milioni za Vicoba Iliyoibiwa Rombo
Taasisi Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kilimanjaro imefaulu kurejesha kiasi cha zaidi ya Sh13.7 milioni zilizofanyiwa ubadhirifu katika kikundi cha Vicoba cha Samaria, kilichopo Kijiji cha Holili.
Fedha hizo zilichukuliwa na mmoja wa viongozi wa kikundi, ambaye baada ya kutokomea, ndugu zake wamebanwa na kurejesha fedha husika.
Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Kilimanjaro ameeleza kuwa ufuatiliaji wa kina ulifanikisha kurejesha fedha zote kwa wanachama husika mwishoni mwa Desemba 2024.
Aidha, Takukuru imefanya uchunguzi wa miradi 26 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh11 bilioni katika sekta ya afya, elimu, maji na ujenzi wa barabara. Uchunguzi huu umebaini mapungufu ya fedha yenye thamani ya Sh3.7 bilioni, hasa katika sekta ya afya na elimu.
Miradi yenye kasoro ilibainisha mipangilio duni ya ujenzi, ama wasimamizi wasio na uwezo wa kutekeleza miradi kwa kiwango cha kutosha.