Kentucky, MAREKANI
MSANII mpya wa kizazi, Omari K, ameweka wazi albamu fupi (EP) yake ya maudhui ya kipekee inayoitwa I AM BANTU MUSIC, itakayotokea siku chache zijazo kwenye majukwaa yote ya muziki.
Omari K ni miongoni mwa wasanii wachache wa Kitanzania wanaoishi Marekani wenye mafanikio makubwa, akiwashirikisha mastaa wa Bongo kama Alikiba na Chino Wanaman kupitia kazi zake za kibubu.
Rapa huyo, mmiliki wa Upendo Records na chombo cha habari, ameshawahi kujipatia mashabiki wengi ndani na nje ya Marekani kwa kutumia lugha mbalimbali ikiwemo Kizigua, Kiswahili na Kingereza.
“I AM BANTU MUSIC ni EP yenye maudhui ya kipekee ambayo itanipa heshima. Mwaka huu nina lengo la kuwakilisha Tanzania vizuri kwenye tasnia ya muziki na filamu hapa Marekani,” alisema.
Zaidi ya muziki, Omari K anaendelea kuandaa filamu mpya inayoitwa Qeen of The Ring, ambayo itaanza kuonyeshwa kwenye cinema Oktoba mwaka huu, akitarajia kushirikisha washabiki wake wa Tanzania, Kenya na Afrika Mashariki.