Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewapongeza wagombea wote wanaoshiriki uchaguzi wa ndani wa chama hicho, akiwakumbusha mambo muhimu ya kuilinda taasisi yao.
Leo, tarehe 13 Januari 2025, Chadema inafanya uchaguzi wa mabaraza ya vijana (Bavicha) na wazee (Bazecha), jambo ambalo limepewa umuhimu mkubwa na viongozi wa chama.
“Leo ni siku muhimu sana kwa Chadema. Napongeza wagombea wote wanaoshiriki. Kila mmoja wenu ni muhimu sana katika kupigania maono ya chama chetu,” ameandika Mbowe.
Ameendelea kusisitiza: “Uchaguzi huu ni zaidi ya nafasi; ni kuhudu mustakabali mzuri kwa Chadema na Taifa letu. Tuna jukumu la kuilinda taasisi yetu na kuhakikisha tunamaliza hatua hii tukiwa imara.”
Mbowe amewahamasisha wanachama na wafuasi kufuatilia mchakato wa kidemokrasia ndani ya chama. “Pamoja, tukiwa na umoja, tutaweza kufanikisha mambo makubwa. Tunaposhirikiana, tunaweza kujenga Chadema yenye nguvu zaidi.”