Habari Kubwa: Maria Sarungi Apatikana Salama Baada ya Kushikiliwa nchini Kenya
Dar es Salaam – Mwanaharakati Maria Sarungi, aliyekuwa ametekwa nchini Kenya, sasa amethibitisha kuwa ana uhai na kuahidi ufafanuzi zaidi kesho.
Taarifa ya kushikiliwa kwake ilitangazwa leo Jumapili, Januari 12, 2025, ikibainisha kuwa alishikiliwa na watu watatu wenye silaha katika eneo la Chaka, Kilimani jijini Nairobi.
Katika taarifa fupi, Maria amesema, “Asanteni sana, nipo salama, Mungu ni mwema. Kesho nitachukua muda, nitaongea, niwashukuru Wakenya, Watanzania na watu wote wa kimataifa. Kwa sababu leo nimeokolewa.”
Hali hii inaendelea kukitisha jamii ya kimataifa, wakitazama matukio yanayoendelea.
Taarifa zaidi itatolewa kesho.