Dar es Salaam: Mwanaume wa Nigeria, Mubarak Bala (40), ameachiwa huru baada ya kuhudumu kifungo cha miaka minne gerezani kwa makosa ya kumtukana Mungu mtandaoni mwaka 2020.
Mubarak alikamatwa Aprili 28, 2020, kwa tuhuma za kukufuru dini na uchochezi kupitia machapisho yake mtandaoni. Aprili 2022, alihukumiwa kifungo cha miaka 24 baada ya kukiri makosa 18, ikiwa ni pamoja na kukufuru na uchochezi.
Januari 7, 2025, aliachiwa huru baada ya kukamilisha kifungo cha miaka minne. Baada ya kuachiliwa, amesema usalama wake bado uko hatarini kutokana na vitisho mbalimbali.
Kwa sasa, anabaki katika mahali salama, huku mawakili wake wakidai kuwa maisha yake yako hatarini ikiwa atarejea kuishi katika jamii ya awali. Hali hii inaonesha changamoto za kubwa za usalama na haki za mtu binafsi katika mazungumzo ya dini na uhuru wa kueleza mawazo.