Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Madiwani wapewa zigo la kuboresha na kujenga mahakama

by TNC
December 3, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Hakimu Mfawidhi Serengeti Aomba Madiwani Kusaidia Ujenzi wa Mahakama

SERENGETI – Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara, Jacob Ndira amewaomba madiwani kusaidia kuboresha mahakama zilizopo na kutenga viwanja kwa ajili ya ujenzi wa mpya na nyumba za mahakimu ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

Ndira alitoa ombi hilo mjini Mugumu Jumatano, Desemba 3, 2025 wakati wa uapisho wa madiwani wateule wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.

Amesema mahakama kama zilivyo taasisi zingine ni sehemu muhimu katika kutoa huduma kwa wananchi.

Hakimu Mfawidhi amesema katika wilaya hiyo baadhi ya majengo ya mahakama yamechakaa na yanahitaji kuboreshwa, akizitaja baadhi zipo kwenye kata za Natta na Kenyana.

"Sisi Mahakama hatujitengi na halmashauri, tunahitaji huduma za madiwani na mfano mzuri ni diwani aliyemaliza muda wake katika Kata ya Robanda amesaidia tumepata jengo zuri la mahakama pale katani kwake, bila kupepesa macho nasema wazi kuwa hakuna jengo zuri la mahakama katika wilaya yetu kama lile la Robanda," amesema Ndira.

Amesema kwa madiwani ambao kata zao hazina mahakama wanapaswa kuanzisha michakato ya kutenga viwanja na ujenzi, akieleza muhimili huo umedhamiria kuwa na mahakama kila kata ili kuboresha na kusogeza karibu na wananchi huduma za taasisi hiyo muhimu katika utawala bora na haki za binadamu.

Makuruma Achaguliwa Tena Kuwa Mwenyekiti

Katika tukio hilo lililokwenda sambamba na uzinduzi wa baraza la tisa la madiwani la halmashauri hiyo, Diwani wa Busawe, Ayubu Makuruma amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa mwenyekiti wa halmashauri kwa kura 40 za ndiyo na moja ya hapana kati ya kura 41 zilizopigwa.

Makuruma anakuwa mwenyekiti pekee aliyemaliza muda wake na kurejea katika nafasi hiyo kati ya wenyeviti wa halmashauri zote tisa za Mkoa wa Mara.

Hilo ni baada ya wenyeviti wengine kushindwa kwenye mchakato wa kura za ndani ya chama au wengine kushindwa kupata nafasi ya kugombea udiwani wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Makuruma amekuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo baada ya jina lake kuwasilishwa na chama chake cha CCM kwa ajili ya kugombea nafasi hiyo na kukosa mpinzani kutokana na chama hicho kupata ushindi katika kata zote 30 za halmashauri hiyo katika uchaguzi mkuu uliopita.

Ahadi za Mwenyekiti

Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Makuruma amesema ili kufikia malengo ya kuleta maendeleo kwa wakazi wa halmashauri hiyo suala la ushirikiano na mshikamano baina ya madiwani, chama na Serikali ni la muhimu.

Kutokana na hilo, amesema atahakikisha jambo hilo linakuwepo kwa kipindi chote cha miaka mitano.

Amesema akiwa mwenyekiti wa halmashauri kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita yapo mafanikio yaliyopatikana na kwamba, matarajio yake ni kuona yanakuwapo mengi na mazuri zaidi.

"Kipindi naingia halmashauri mapato yetu yalikuwa ni Sh980 milioni lakini hadi tunamaliza muda wetu wa uongozi na utumishi wa wananchi mapato yetu yalipanda na kufika Sh6.6 bilioni, tutarajie kupanda zaidi," amesema Makuruma.

Amesema atahakikisha kunakuwapo usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha za Serikali kuu, mapato ya ndani na wahisani ili miradi hiyo iwe na tija kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.

Kuhusu masilahi ya madiwani, Makuruma amesema wakati anaingia madarakani posho yao ilikuwa Sh150,000 lakini hadi wanaondoka waliongeza kiwango hadi kufika Sh420,000.

Amesema hadi baraza la madiwani lilipovunjwa, hakuna diwani aliyekuwa akiidai halmashauri hiyo.

Ili kuongeza pato la ndani la halmashauri, amesema wanatarajia kuibua vyanzo vingine vipya vya mapato, ikiwa ni pamoja na kutumia fursa ya utalii kupitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, hatua itakayosababisha halmashauri kuwa na uwezo wa kutekeleza miradi mingi na mikubwa kwa masilahi ya wananchi.

Katika uchaguzi huo, Diwani wa Rung’abure, Elias Mwita, amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri kwa kupata kura zote 41 zilizopigwa.

Tags: kuboreshaKujengaMadiwanimahakamaWapewazigo
TNC

TNC

Next Post

Tanzania's DPP drops treason charges, releases cosmetics entrepreneur 'Niffer' and Mika Lucas Chaval

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company