Tuesday, December 9, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Wahitimu wapewa mbinu kukabili tatizo la ajira kidijitali

by TNC
November 30, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Wahitimu Watakiwa Kutumia Teknolojia Kutatua Changamoto za Ajira

Arusha. Wakati Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) likionyesha zaidi ya asilimia 50 ya wahitimu katika ukanda huo hawapati ajira, wahitimu wametakiwa kutumia teknolojia kujenga mifumo bunifu na salama inayotatua changamoto za kwenye jamii kama nyenzo muhimu ya kutengeneza uchumi.

Kulingana na uchunguzi wa IUCEA, ukosefu wa ujuzi unaohitajika katika sekta muhimu, hususan huduma, mawasiliano, teknolojia, na ufundi wa kazi mbalimbali ndio sababu kuu ya ukosefu wa ajira.

Takwimu zinaonyesha kuwa miongoni mwa wahitimu, asilimia 51 hukosa ajira nchini Kenya, asilimia 55 nchini Burundi, na asilimia 52 nchini Rwanda. Nchini Tanzania asilimia 61 ya wahitimu hawana ajira, na nchini Uganda asilimia 63 hawana ajira.

Akizungumza katika mahafali ya 23 ya Chuo cha Usimamizi cha Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI), yaliyohitimisha wahitimu 350 wa ngazi za cheti, stashahada na shahada ya uzamili katika uongozi, Mkurugenzi wa ESAMI, Dk Peter Kiuluku, amesema kuwa hali hiyo ni tishio kubwa kwa utulivu wa kisiasa, maendeleo, na ustawi wa kiuchumi wa eneo.

"Zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya watu Afrika ni chini ya miaka 35, na robo tatu kati yao hawana ajira. Leo mmehitimu hapa nendeni mkatumie teknolojia kama nguzo kuu ya ubunifu katika kutatua changamoto za jamii. Hiyo ndio itakayowapatia uchumi endelevu, badala ya kuongeza idadi ya wasio na ajira," amesema Dk Kiuluku.

Dk Kiuluku amesema kuwa wahitimu hao, kutoka nchi 41 za Afrika, wanatarajiwa kuwa wachochezi wa kuunda ajira kupitia fursa bunifu watakazozitafuta.

Waziri wa Elimu wa Zambia, Douglas Munsaka, akihutubia wahitimu, amesema umuhimu wa mataifa ya Afrika kukabiliana na ukosefu wa ajira kupitia maendeleo ya kiteknolojia.

"Katika miaka 10 pekee, dunia imebadilika kwa kasi kupitia majukwaa ya kidijitali, data kubwa, na akili bandia (AI). Ubunifu si anasa tena ni nguvu kuu ya maendeleo ya kisasa. Mataifa yanayofanikiwa ni yale yanayoweza kutumia teknolojia kwa njia ya kimaadili, kiuwajibikaji, na kimkakati," amesema Munsaka.

Munsaka amewataka wahitimu kuwa viongozi wanaoweza kutafsiri teknolojia kwa manufaa ya wananchi wao, na kuunganisha maadili ya Kiafrika na suluhisho za kiteknolojia katika uongozi, utawala, na maendeleo ya jamii.

Mhitimu Theresia Mtewele, aliyehitimu shahada ya uzamili katika uongozi wa biashara, amesema elimu aliyopata imewezesha kuongoza mageuzi ya utawala kwa kutumia AI, kuboresha uwazi na ufanisi katika taasisi za umma na binafsi.

Mtewele amewahimiza wenzake kuchapisha tafiti zao ili ziwe rejea muhimu kwa jamii na dunia, kwani zinasaidia kubaini changamoto, kutoa suluhisho, na kuendeleza matokeo ya ubunifu katika sekta mbalimbali.

"Afrika ina kila sababu ya kukimbiza kasi ya dunia. ESAMI imetupa misingi ya kufanya hivyo," alisema.

Tags: AjiraKidijitalikukabiliMbinuTatizowahitimuWapewa
TNC

TNC

Next Post

Viongozi wa ushirika watakiwa kuzingatia sheria, kuimarisha uadilifu

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company