Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Vijana waeleza matumaini yao kuanzishwa kwa Wizara ya Vijana

by TNC
November 30, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Wahitimu wa CBE Wapongeza Uanzishwa wa Wizara ya Vijana

Mbeya – Wahitimu wa Chuo cha Biashara (CBE) wamepongeza uwapo wa Wizara ya Vijana wakitaja kuwa ni suluhisho la changamoto zao huku wakishauri mambo yatakayosaidia kumaliza tatizo la ajira na kuweka ustawi bora wa kundi hilo.

Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza kuunda wizara hiyo huku Joel Nanauka akiteuliwa kuwa Waziri katika wizara hiyo na tayari amefanya ziara katika mikoa ya Songwe, Mbeya na Ruvuma kusikiliza kero za vijana nchini.

Wakizungumza Novemba 29, 2025 wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho kampasi ya Mbeya, wahitimu hao wamesema kwa miaka ya nyuma, kundi la vijana lilisahaulika kwa kuchanganywa na makundi mengine.

Mansura Mussa, mhitimu wa stashahada ya Biashara, amesema kuwepo kwa Wizara ya Vijana kutasaidia kundi hilo kufikisha mahitaji kwa uharaka, akiomba uwapo wa mazingira mazuri kwa wanaojiajiri.

"Kama ni mikopo ya kutuinua kiuchumi itufikie, kusiwepo utitiri wa kodi hasa kwa vijana ambao tumeajiajiri, mazingira yawe rafiki," amesema Mansura.

Kwa upande wake, Yohana Mtimila amesema licha ya matumaini ya uwapo wa wizara hiyo, ifanye utafiti wa makundi ya wasomi, wabunifu na wale wasio na elimu kujua mahitaji yao ili kuweka ustawi bora kwa vijana.

Ameongeza kuwa elimu waliyopata wataitumia kama daraja kutafuta fursa za kujikwamua kiuchumi ili kuendesha maisha yao, akibainisha kuwa biashara na elimu ni vitu vinavyotegemeana.

"Tumepata ujuzi ambao unaweza kutusaidia kujiajiri badala ya kuisubiri serikali, bila elimu biashara inakuwa ngumu, wizara isaidie kubaini uhitaji wa waliosoma na wenye ubunifu kuwakwamua," amesema Mtimila.

Naye Naomi Simkombe amewaomba wahitimu kutumia elimu waliyoipata kuwa daraja la kufikia mafanikio kwa kujiajiri kupitia mitandao na kutochagua wala kubagua kazi kwa kigezo cha elimu ya juu.

"Tunaamini serikali kupitia Wizara ya Vijana itasaidia kuweka mazingira mazuri, lakini wahitimu wenzangu wasichague kazi huko mtaani, watumie mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zao," amesema Naomi.

Akizungumza katika mahafali hayo kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Hashim Abdallah amewataka wahitimu kuwa waadilifu huko uraiani.

Amesema serikali imefanyia maboresho ya kisekta na kisera katika upande wa Viwanda na Biashara na Elimu ikiwa ni kuanzisha mtaala mpya na programu ya Samia Scholarship kwa kuongeza fedha za mikopo kwa ngazi za shahada ya awali na stashahada.

"Hali hii imeongeza wanafunzi wengi kujiunga na vyuo, kipekee nipongeze uongozi wa chuo hiki kwa mafanikio ikiwamo ukuaji wake kikanda na kuwa chuo cha nane kati ya vyuo 47 vya elimu ya juu," amesema.

"Serikali ina imani kubwa na CBE katika kutoa mchango kwa jamii kwa kutoa elimu ya biashara na usimamizi, utafiti na ushauri kitaalamu jinsi ya kuendesha biashara kama nyenzo muhimu kutekeleza Sera ya Viwanda na Biashara," amesema Dk Abdallah.

Ameongeza kuwa kuhusu changamoto zilizoainishwa ikiwamo uhaba wa watumishi, serikali inaenda kuzifanyia kazi na kuzipatia ufumbuzi, na itaendelea kuweka mazingira mazuri na wezeshi ili kuifikia jamii zaidi.

"Tumefurahishwa na mipango ya chuo na endeleeni kukuza uanagenzi, ujasiliamali na uatamizi ili kufikia kundi kubwa la Watanzania kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla."

Tags: KuanzishwakwaMatumainivijanaWaelezaWizarayao
TNC

TNC

Next Post

Chama cha siasa chamlilia mbunge wake wa zamani

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company