Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Mwanachuo anayedaiwa kujeruhi adai video iliyosambaa mtandaoni imetengenezwa

by TNC
November 27, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mshtakiwa wa Kesi ya Ujeruhi Adai Video za Ushahidi Zimetengenezwa

Dar es Salaam – Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mary Matogolo (22), anayekabiliwa na kesi ya kujeruhi, amedai video zinazomuonyesha akiwa chumbani kwake eneo la Sinza, Dar es Salaam na wenzake wakimjeruhi mwenzao siyo halisi, bali za kutengenezwa.

Vilevile, amedai washtakiwa wengine katika kesi hiyo hawafahamu zaidi ya kukutana nao Kituo cha Polisi Oysterbay na kuunganishwa pamoja katika mashtaka hayo.

Matogolo ameeleza hayo leo Novemba 26, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alipotoa utetezi baada ya mahakama kutoa uamuzi kuwa pamoja na wenzake wawili wana kesi ya kujibu.

Ametoa ushahidi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga.

Washtakiwa wengine ni Ryner Mkwawili, mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi na Asha Juma, wa Chuo cha Uhasibu Dar es Salaam (TIA).

Mashtaka Yanayowakabili

Kwa pamoja washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka manane, yakiwamo ya kumsababishia madhara kimwili mwanafunzi mwenzao, Magnificant Kimario, kutishia kuua, kutoa taarifa za uongo mitandaoni na uharibifu wa mali.

Akiongozwa na wakili, Peter Shapa, mshtakiwa Matogolo ameimba mahakama imuondolee mashtaka yanayomkabili na imwachie huru kwa sababu hahusiki na kesi hiyo.

"Hata video ambazo zinanionyesha nikiwa chumbani kwangu eneo la Sinza, nikiwa na wenzangu tunamjeruhi Magnificant, si halisi kwani zimetengenezwa," amedai.

"Hata washtakiwa wengine ambao wapo katika kesi hii, siwafahamu zaidi ya kukutana nao Kituo cha Polisi Oysterbay na kuunganishwa pamoja katika mashtaka haya," ameongeza.

Amekana kuhusika kuchapisha taarifa za uongo na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii ambazo zinaonyesha alivyoshirikiana na wenzake kumpiga Magnificant Kimario.

Vilevile, amedai hajawahi kuishi chumba kimoja na Magnificant wala hamfahamu zaidi ya kukutana naye Kituo cha Polisi Oysterbay.

Maswali ya Dodoso

Akihojiwa maswali ya dodoso na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Gabriel Kamugisha, alikiri kuyatambua maelezo ya onyo kuwa ni yake.

Wakili Kamugisha alimuonyesha sehemu katika maeneo hayo na kumtaka asome. Sehemu hiyo inaeleza namna alivyoonekana kwenye video hizo na aliikiri kuonekana, lakini akidai siyo halisi, bali imetengenezwa.

Ushahidi wa Mshtakiwa wa Pili

Kwa upande wake, shahidi wa pili wa upande wa utetezi, Ryner Mkwawili ambaye ni mshtakiwa katika kesi hiyo amedai anamtambua mlalamikaji (Magnificant) na kwamba walishawahi kusoma darasa moja.

Amedai wakati wa tukio likitendeka alikuwa amesafiri kwenda mkoani kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka. Amedai tuhuma zinazomkabili si za kweli, hivyo anaomba mahakama imuachie huru.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho Novemba 27, 2025 itakapoendelea kusikilizwa shahidi wa upande wa utetezi.

Maelezo ya Mashtaka

Katika shtaka la kwanza, washtakiwa wote wanadaiwa Machi 16, 2025, eneo la Sinza, wilayani Ubungo walikula njama kwa nia ya kutenda kosa la kuchapisha taarifa za uongo.

Shtaka la pili linawakabili Mary na Asha wanaodaiwa siku hiyohiyo walisambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa WhatsApp yenye maneno: "Toa sauti umefanya mapenzi na Mwijaku lini na wapi."

Ryner, katika shtaka la tatu anadaiwa siku hiyohiyo alisambaza taarifa ya uongo kupitia mtandao wa WhatsApp.

Shtaka la nne la kusababisha madhara linamkabili Mary anayedaiwa siku hiyohiyo alimshambulia Magnificant Kimario kwa kumpiga kichwani kwa chuma na kumsababishia maumivu makali.

Washtakiwa wote katika shtaka la tano wanadaiwa kwa kutumia nguvu walimvuta nywele Magnificant na kumsababisha madhara makubwa.

Katika shtaka la sita na la saba, Mary anadaiwa kuharibu laini ya simu na simu aina ya Samsung yenye thamani ya Sh700,000, mali ya Magnificant.

Shtaka la nane linawakabili washtakiwa wote wanaodaiwa walitishia kumuua Magnificant kwa kutumia kisu.

Washtakiwa wote wamekana mashtaka hayo na wako nje kwa dhamana. Kwa mara ya kwanza, walifikishwa mahakamani hapo Mei 30, 2025 na kusomewa kesi ya jinai namba 13199 ya mwaka 2025.

Tags: adaiAnayedaiwailiyosambaaimetengenezwaKujeruhiMtandaoniMwanachuoVIDEO
TNC

TNC

Next Post

Madaraja yanayounganisha mikoa ya kusini kukamilika Desemba 24

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company