Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Matumizi ya gesi asilia yanavyoongeza mapato

by TNC
November 26, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mapato ya Gesi Asilia Yaongezeka Mara Mbili Tanzania

Dar es Salaam – Ukuaji wa matumizi ya gesi asilia maeneo mbalimbali nchini umetajwa kuwa sababu ya kukua kwa mapato yatokanayo na nishati hiyo inayozalishwa eneo la Songosongo na Mnazi Bay, Ripoti ya Tanzania Abstract 2024 inaeleza.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya hivi karibuni iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mapato ya gesi asilia yamefikia Sh358.192 bilioni mwaka 2024 kutoka Sh137.013 bilioni mwaka 2020.

Hilo ni sawa na ongezeko la zaidi ya mara mbili huku mageuzi ya kuelekea nishati safi yanayochochea matumizi ya gesi ya kupika, magari, kuzalisha umeme na kuendeshea viwanda, yakitajwa kuwa sababu ya ukuaji wa mapato hayo.

Mchambuzi huru wa masuala ya fedha, Oscar Mkude amesema hayo ni matokeo ya uwekezaji unaofanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kupanua mtandao wake wa usambazaji wa gesi.

Mbali na kusambaza gesi kwa ajili ya uzalishaji wa umeme Kinyerezi, sasa shirika hilo linapeleka gesi katika viwanda mbalimbali vikiwamo Kiwanda cha Dangote.

Matumizi ya CNG Yameongezeka Kwa Kasi

"Kadri mtandao huo unavyozidi kukua, viwanda vingi vimeanza kubadili mfumo na kutumia gesi asilia, matumizi ya CNG yameongezeka kwa kasi, hasa baada ya kuyumba kwa bei za mafuta kunakohusishwa na mvutano kati ya Russia na Ukraine," amesema Mkude.

Mkude amesema ongezeko la matumizi ya gesi asilia viwandani linatarajiwa kuongeza mapato ya serikali kwa sababu nishati hiyo inatumika kila siku na pikipiki za magurudumu matatu (bajaj) pamoja na huduma nyingine za usafiri barabarani.

Amesema hiyo itakuwa na manufaa pia katika kuokoa fedha za ndani, kwa kuwa sasa Tanzania inaagiza mafuta kutoka nje na wakati wa upungufu huathiriwa mabadiliko ya bei hali inayogusa uchumi moja kwa moja.

"Uongezaji wa matumizi ya CNG umetoa mbadala muhimu na kusaidia kupunguza shinikizo kwenye akiba ya fedha za kigeni. Mabadiliko yalianza na bajaji kuhamia CNG, kisha magari binafsi na sasa hata mabasi ya mwendokasi (BRT)," amesema.

Mkude amesema mradi wa ubadilishaji wa gesi kuwa kimimika utakapoanza kazi (LNG), utaleta mabadiliko makubwa katika uchumi kwa kuwezesha Tanzania kuuza nje kwa wingi na kupata fedha za kigeni kwa kiasi kikubwa.

Faida za Mazingira na Kiuchumi

Mtaalamu wa Uchumi, Profesa Abel Kinyondo amesema kuna faida mbili za gesi asilia, kwanza ni chanzo safi cha nishati ukilinganisha na petroli, dizeli na mafuta ya taa.

"Ingawa si nishati safi zaidi kuliko zote, ni safi kwa kiwango kikubwa kuliko mafuta ya kawaida. Pili, gesi ni nafuu zaidi na kadiri miundombinu inavyozidi kupanuka, unafuu wake na manufaa yake kimazingira yanazidi kuimarika," amesema.

"Kuongezeka kwa upatikanaji kutahamasisha matumizi mapana zaidi, hivyo kuiwezesha Tanzania kusonga mbele kuelekea kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo 2050."

Upanuzi wa Mtandao wa Usambazaji

Kukua kwa mtandao wa matumizi ya gesi pia kulitajwa katika bajeti ya Wizara ya Nishati ya mwaka 2025/26 ikionesha kwamba, kuwapo kwa ongezeko la mtandao wa usambazaji wa gesi asilia nchini kutoka kilomita 102.54 mwaka 2020/21 hadi kilomita 241.58 Aprili 2025.

Imeelezwa kuwa, kukua kwa mtandao huo kumewezesha kuunganishwa kwa jumla ya nyumbu 1,514, taasisi 13 na viwanda 57.

Pia, zaidi ya vyombo vya moto 15,000 vinatumia gesi asilia, hivyo kupunguza mahitaji ya petroli na dizeli katika uendeshaji wa vyombo vya moto nchini.

Hilo limeenda sambamba na kuongezeka kwa matumizi ya gesi asilia nchini kutoka futi za ujazo bilioni 59.83 mwaka 2020/21 hadi futi za ujazo bilioni 82.91 Aprili 2025.

Ahueni kwa Wananchi na Biashara

Kupanuka kwa mtandao huo pia kumeleta ahueni kwa watu wengi ikiwamo wananchi na watoa huduma wa vyombo vya moto kwa kuwa, umesaidia kupunguza gharama za maisha na uendeshaji wa biashara kwa jumla.

Hiyo ni baada ya bei ya gesi kutoathiriwa na yale yanayoendelea duniani ikiwemo machafuko yoyote ikilinganisha na inavyokuwa kwenye mafuta.

"Gesi kilo moja ni Sh1,550 nikiwa na mtungi wa kilo 15 wa gesi asilia kwenye gari langu ni takribani Sh23,000 ukilinganisha na lita moja ya mafuta ambayo kwa sasa ni kama Sh2,752 inategemeana na sehemu utakayonunua unaweza kuaona ni kiasi gani tumeokoa," amesema Suleiman Sulehly ambaye ni dereva.

Amesema awali, walikuwa wakipata unafuu wa bei, lakini wakitumia muda mwingi kusubiri kujaza gesi jambo ambalo sasa limefikia ukomo baada ya kushuhudiwa ongezeko la vituo katika Jiji la Dar es Salaam.

"Hakuna kusubiri tena, mtu ulikuwa unalazimika kwenda kituoni usiku wa manane kama hautaki kupoteza muda wa kazi, lakini sasa tuna uhuru wa kwenda katika kituo, kwanza unachagua ujazo wake, yale mawazo kuwa hadi uende Tazara au Ubungo au Uwanja wa Ndege sasa hivi hayapo vituo vimekuwa vingi," amesema Sulehly.

Mbali na kuona faida katika biashara, kwa watumiaji wa gesi hiyo kwa kupikia, wanasifu kilichofanyika kwa kuwa, sasa hawana ulazima wa kuwa na kiwango kikubwa cha fedha ili wapike badala yake wanatumia kidogokidogo.

"Kama umeme, kadri unavyonunua ndiyo unavyotumia, gesi ya mitungi ikipanda bei sisi tunasikia tu, malalamiko kwa wengine, sisi hatuumii kabisa tumeshaondoka kwenye huo msongo wa mawazo," amesema Leah Mzee mkazi wa Mlalakuwa.

Tags: asiliaGesimapatoMatumiziyanavyoongeza
TNC

TNC

Next Post

Mwanachuo anayedaiwa kujeruhi adai video iliyosambaa mtandaoni imetengenezwa

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company