Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Wafanyabiashara watakaonunua parachichi mashambani kudhibitiwa Rungwe

by TNC
November 20, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mbeya. Katika jitihada za kudhibiti wanunuzi holela wa zao la parachichi mashambani, Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya, imekuja na mkakati wa kuanza ujenzi wa mradi wa vituo saba vya kukusanyia kabla ya kuingizwa sokoni.

Mradi unatekelezwa na Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana halmashauri hiyo, kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA).

Imeelezwa kati ya vituo saba, viwili vinajengwa Busokelo na vitano Rungwe mkoani hapa kwa lengo la kuwezesha wakulima kuwa na sehemu moja ya kuuzia ili kudhibiti walanguzi wanaowafuata mashambani.

Ofisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Rungwe, Adam Salum amesema ujio wa mradi utakuwa suluhisho kwa wakulima kuzalisha kwa tija na kuuza zao la parachichi kwa bei nzuri ya kujikwamua kiuchumi.

"Tayari mradi huo umeanza katika halmashauri mbili za Busokelo na Rungwe, lakini ukikamilika utakuwa chachu ya wakulima kujiongezea mapato na kuchangia mapato ya halmashauri," amesema.

Salum amesema kwa kipindi cha mwaka 2024/2025, uzalishaji wa parachichi umeongezeka kutoka wastani wa tani 25,866 mpaka 30,642, sawa na asilimia 64.7.

Amesema ongezeko hilo limetokana na mwitikio mkubwa wa wakulima kuwekeza kwenye kilimo sambamba na elimu ya wataalamu katika kuandaa vitalu vya miche mpaka hatua ya uzalishaji.

"Mwitikio ni mkubwa licha ya hapo awali kuwepo kwa changamoto ya masoko makubwa ya nje, lakini Serikali inaendelea kuona namna bora ya kuwasaidia hususani ujenzi wa miundombinu ya kisasa yenye baridi na viwanda vidogo vya kuongeza thamani," amesema.

Amesema kwa msimu uliopita zao hilo lilichangia mapato ya halmashauri zaidi ya Sh400 milioni ambazo zilielekezwa kwenye miradi mbalimbali hususani ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Avocado.

"Parachichi ni zao kuu linalоchangia mapato ambayo tunaelekeza kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo sambamba na kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji kufikisha sokoni," amesema.

Mkulima wa parachichi Kata ya Kiwira, Estrida Joel amesema endapo Serikali ikaharakisha ujenzi wa vituo hivyo utakuwa mkombozi kwao kwani kuna kipindi mazao hufika kuharibika kwa kukosa masoko na hata ukipata tunauza bei rahisi.

"Kimsingi tumekuwa tukinyonywa na wanunuzi kwa kujipangia bei wakifika mashambani jambo ambalo tunalazimika kukubaliana nao kwani hakuna masoko ya uhakika na tunaomba Serikali kuwatafutia masoko mbadala wakati ujenzi wa vituo ukiendelea," amesema.

Tags: kudhibitiwamashambaniParachichiRungweWafanyabiasharawatakaonunua
TNC

TNC

Next Post

Al Barakah Sukuk oversubscribed as investor appetite for Islamic finance grows

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company