Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji latangaza nafasi za ajira

by TNC
November 19, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
131
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Jeshi la Zimamoto Latangaza Nafasi Mpya za Ajira kwa Vijana

Dar es Salaam – Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini limetangaza nafasi mpya za ajira kwa vijana wa Kitanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano Novemba 19, 2025, ajira hizo zinawalenga vijana wenye sifa za kuanzia elimu ya kidato cha nne, kidato cha sita, stashahada hadi shahada.

Taarifa hiyo imesainiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga, ni kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sura ya 427 na Kanuni za Utumishi za mwaka 2008.

Masharti kwa Waombaji wa Kidato cha Nne

Taarifa hiyo imeleza waombaji wa elimu ya kidato cha nne wanatakiwa kuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, wenye afya njema, bila kumbukumbu za uhalifu, wasiokuwa wameoa au kuolewa, na wenye umri wa miaka 18 hadi 25.

Masharti mengine ni kutokuwa na alama za kuchora mwilini, kutotumia dawa za kulevya, na kuwa tayari kuhudhuria mafunzo ya taaluma ya Zimamoto na Uokoaji.

Nafasi Zilizotangazwa

Taarifa hiyo imeweka wazi kuwa ngazi ya kidato cha nne na sita, nafasi zilizotangazwa zinahusu madereva wa magari makubwa, wauguzi, wataalamu wa Zimamoto na Uokoaji, matabibu, mafundi mchundo wa magari, wazamiaji na waogeleaji, wanamichezo, wanamuziki wa brass band, waandishi waendesha ofisi, wataalamu wa Tehama na mafundi umeme wa ndege.

Aidha, waombaji wote hao wanatakiwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 28, huku madereva wakihitajika kuwa na leseni daraja E na watafanyiwa uhakiki wa vitendo.

Nafasi kwa Wenye Shahada

Kwa ngazi ya shahada, nafasi zimetolewa kwa wahandisi bahari, wahandisi wa Tehama, wahandisi wa ndege, wakadiriaji majengo (QS), wataalamu wa sheria waliomaliza shule ya sheria kwa vitendo, wahandisi mafuta na gesi, wahandisi ujenzi, mitambo na umeme.

Waombaji wa nafasi hizo nao wanatakiwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 28 na sifa zote za msingi.

Jinsi ya Kuomba

Taarifa hiyo inaelekeza kuwa maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo wa ajira wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia tovuti ya https://ajira.zimamoto.go.tz kabla ya Desemba 03, 2025.

Aidha, waombaji wanatakiwa kuambatisha barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono, fomu ya uthibitisho wa afya kutoka kwa mganga wa Serikali, nakala ya kitambulisho cha Taifa (Nida), namba za mitihani ya kidato cha nne na sita, vyeti vya taaluma vinavyotambulika na serikali, pamoja na barua ya utambulisho kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa.

Jeshi hilo limeeleza kuwa barua zitakazowasilishwa kwa njia ya posta, mkono au barua pepe hazitapokelewa.

Aidha, imesisitizwa kuwa nakala za vyeti vingine lazima ziwe zimeidhinishwa na kamishna wa viapo au hakimu na waombaji wote wanatakiwa kuandika namba za simu kwenye barua zao za maombi.

Onyo kwa Waombaji

Jeshi limetoa onyo kuwa yeyote atakayewasilisha nyaraka za kughushi au taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kisheria.

Tags: AjiraJeshilatangazanafasiUokoajiZimamoto
TNC

TNC

Next Post

Police confirm Tanzanian comedian MC Pilipili was murdered

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company