Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Watanzania wahamasishwa kuhubiri haki ili kuilinda amani

by TNC
November 17, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Jamii Yashauriwa Kumrudia Mungu Kwa Kulinda Amani

Njombe – Jamii ya Watanzania imeshauriwa kumrudia Mungu kwa kuhakikisha inatenda mambo mema na kuhubiri haki ili kutunza na kuilinda amani iliyopo hapa nchini.

Ushauri huo umetolewa Novemba 16, 2025 na Mwinjilisti wa Kanisa la Waadventisti Wasabato, Mkoa wa Njombe, Andrew Chikwanda wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe.

Mwinjilisti huyo ameyasema hayo zikiwa zimepita siku 18 tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu uliotawaliwa na maandamano yaliyozua vurugu zilizosababisha vifo, uharibifu wa mali za umma na binafsi.

Amesema ukaidi wa kuzitekeleza amri 10 za Mungu kwa wanadamu umesababisha madhila yanayotokana na nguvu ya shetani inayopandikizwa kwa watu.

Amesema vitendo vinavyofanywa na wanadamu hivi sasa ni chukizo machoni mwa Mungu, hivyo kila mmoja anapaswa kumrudia kwa kutenda mema na kuhubiri haki.

Amesema kwa kufuata na kutekeleza amri za Mungu, jamii itatenda haki na kuvumiliana katika masuala mbalimbali hivyo na amani itaendelea kuwepo nchini.

"Hapo zamani familia zilikuwa zinajua kuwalea watoto wao ili wawe na heshima kwa watu wanaowazunguka na neno la Mungu linawajenga vijana na watoto kuwaheshimu binadamu wenzao," amesema Chikwanda.

Amesema matukio mengi mabaya yanayotokea katika maeneo mbalimbali duniani ni kwa sababu ya watu kumsahau Mungu na kutenda mambo maovu yasiyompendeza Mungu.

Kwa upande wake, Mwinjilisti Joseph Mungale wa Kanisa la Waadventisti Wasabato amesema vijana wakimfuata Mungu kwa kutii neno lake wataweza kuepukana na changamoto ambazo zinawakabili.

"Vijana wanatakiwa kutii upande wa Serikali lakini pia upande wa Mungu kwani ukiharibu upande mmoja lazima na mwingine uharibu," amesema Mungale.

Mkazi wa Njombe, Christina Mange amesema vijana wana nafasi kubwa ya kubadilisha taifa endapo watafuata neno la Mungu na kuishi kwa kufuata maadili mema.

"Tunaishi katika ulimwengu ambao umechanganyikiwa hivyo hivyo tuishi katika maelekezo ya Mungu kwani tuna nafasi ya kuliandaa na kulisaidia taifa katika changamoto nyingi linalopitia," amesema Mange.

Tags: amaniHakiilikuhubirikuilindaWahamasishwaWatanzania
TNC

TNC

Next Post

Sajenti wa Jeshi akamtwa akiwa na mabomu manne

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company