Sunday, December 7, 2025
  • Login
No Result
View All Result
Instagram
TNC
  • Home
  • Home
No Result
View All Result
TNC
No Result
View All Result

Watumishi wa umma jengeni tabia ya kupima afya

by TNC
November 15, 2025
in Swahili
0
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Shinyanga: Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro amewahimiza wananchi wa wilaya ya Shinyanga hususani watumishi wa umma kujenga tabia ya kupima afya mara kwa mara kwani kutokufanya hivyo kunasababisha magonjwa ambavyo yangeweza kutibika mapema kuchukua muda mrefu na gharama.

Akizungumza Novemba 15, 2025 katika kikao cha uwasilishaji taarifa ya lishe kwa Manispaa ya Shinyanga, kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa mkoani Shinyanga, Mtatiro ameeleza kuwa ni vyema jamii ikabadilika na kujenga tabia ya kufanya vipimo mara kwa mara.

"Watumishi wa Umma jengeni tabia ya kupima afya, ni muhimu zaidi tukajenga tabia ya kufanya vipimo vya afya zetu mara kwa mara sio hadi uugue ndipo uende hospitali kwa ajili ya matibabu, watumishi wa Umma tuwe mfano wa kuigwa kwa wananchi tujali afya zetu kwani ndiyo kila kitu," amesema Wakili Mtatiro.

Pia ameongeza kuwa, "Wakina mama mnatakiwa kupima saratani ya shingo ya kizazi angalau mara moja kwa kila miaka miwili ugonjwa huu umekuwa ni tatizo na mengi pia yamekuwa yakisababishwa na msongo wa mawazo ni vyema jamii ikabadilika."

Kwa upande mwingine Mtatiro amewataka wataalamu wa afya kutoa elimu ya mara kwa mara kwa watumishi pamoja na wananchi wote ili wachukue tahadhari mapema ya magonjwa hatari katika jamii pamoja na kusisitiza juu ya masuala ya lishe bora katika jamii.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa lishe kwa Manispaa ya Shinyanga, Mratibu wa Lishe Misango George amesema katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2025, jumla ya watoto 135 walibainika kuwa na utapiamlo.

"Kati ya watoto walioandikishwa watoto 135 waligundulika kuwa na utapiamlo na watoto 122 wamepona na waliobaki wanaendelea na matibabu katika hospitali na vituo vya afya katika Manispaa ya Shinyanga," amesema George.

Wakichangia taarifa hiyo wajumbe wameshauri kuendelea na mikakati ya kuhamasisha shughuli za lishe shuleni na kwenye jamii ili kufikia lengo la mkataba wa lishe.

Tags: AfyaJengenikupimaTabiaUmmaWatumishi
TNC

TNC

Next Post

Why climate loss and damage financing is a health imperative

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Popular News

  • Zanzibar’s Leadership Advocates for Streamlined Tax System to Enhance Economic Growth

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanaohujumu miundombinu watachukuliwa hatua kali

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wasiwasi juu ya Uchochezi wa Makada katika Jimbo la Katavi

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Wanawake Wanaonyonyesha Washauriwa Kula Milo Mitano Siku

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Category

  • English
  • Swahili

Socials

Instagram TikTok YouTube Facebook

About Us

TNC (Tanzania News Company) is the primary Source of News in English & Swahili in Tanzania

© 2025 TNC - Tanzania News Company

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home

© 2025 TNC - Tanzania News Company